KUMBILAMOTO KIDEDEA UCHAGUZI NAIBU MEYA ILALA.
Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto akipiga kura leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala wamefanya uchaguzi wa kumchagua naibu meya baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Omary Kumbilamoto kujiudhuru kwa kuhama Chama cha Wananchi (CUF) kwenda CCM.
Uchaguzi huo umefanyika leo ambapo wajumbe 52 wameshiriki kupiga kura kumchagua naibu meya wa Manispaa ya ilala jijini Dar es Salaam.
Wagombea katika uchaguzi huo ni Diwani wa kata ya Vingunguti (CCM) Omary Kumbilamoto, Diwani Kata ya Buguruni (CUF) Adamu Rajabu Fugame pamoja diwani wa kata ya Tabata kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Patric Assenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi Msimamizi wa Uchaguzi huo Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Jabiri Makame, amesema kuwa ujumla ya wapiga kura walikuwa 52 na hakuna kura yoyote iliyoharibika.
Amesema kuwa mgombea Patric Assenga hakupata kura yoyote, Rajabu Fugame amepata kura 25 huku Omary Kumbilamoto akipata kura 27.
Kutokana na matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto kuwa mshindi wa uchaguzi wa kiti cha naibu meya Manispaa ya Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kuwa mshindi Kumbilamoto, amewashukuru wajumbe waliompigia kura huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kikamilifu.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kuwa mshindi Kumbilamoto, amewashukuru wajumbe waliompigia kura huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kikamilifu.

Post a Comment