ACT WAZALENDO WAICHAMBUA SEKTA YA ELIMU NCHINI
Serikali imetakiwa
kutoendelea kujitapa kwa kuweka fedha nyingi katika ujenzi wa madarasa, bali
imetakiwa kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya watoto kujisomea pamoja na
maslahi ya walimu ili watoe elimu bora.

Hayo yamesemwa
mapema leo jijini Dar es salaam na msemaji wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu
Addo Shaibu wakati akitoa tathmini ya hali ya elimu hapa nchini.
Ndugu Addo
alisema kuwa kiwango cha elimu nchini kimeshuka na kusababisha wanafunzi wengi
hasa wa shule ya msingi kutojua kusoma na kuandika, kwani hapo mwanzo darasa
moja ililitakiwa kuwa na wanafunzi 48 kwa mwalimu mmoja lakini kwa sasa
wanafunzi 52 na zaidi hali inayoonyesha walimu kuelemewa.
Aliendelea kusema
kuwa sababu ya walimu kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ni kuwa na
malimbikizo mengi ya mishahara yao, kukosa nyumba za kuishi, kukosa nyenzo za
kufundishia na n.k hali inayosababisha walimu kushindwa kufanya kazi kwa weledi
na hatimaye kuvujisha mitihani ili kupata mahitaji yao muhimu.
Na mwisho
kabisa alipenda kuishauri serikali kuweza kutoa takwimu sahihi kuhusiana na
hali ya elimu hapa nchini, lakini pia kuwapa ajira walimu wenye vigenzo na
kuangalia elimu bora na siyo kuangalia matokeo ya vyeti kwani mtu anaweza
kununua na kwenye ufanisi akawa mbovu vilevile.
Post a Comment