Kubenea: Naweza Kuhama CHADEMA Muda Wowote Nikiamua

Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea amefunguka kuwa yeye kutohudhuria kwenye zoezi la uzinduzi wa kitabu cha sera za Chama hicho haimaanishi kuwa anataka kundoka kwani kuondoka ni maamuzi na anaweza tekeleza muda wowote.
Kubenea
amesema kuwa katika uzinduzi wa sera halikuwa jambo la lazima, na
alikuwa katika utekelezaji wa majukumu mengine hivyo wanaohoji
kutoshiriki kwake ni watu waliopo kwaajili ya kumchafua.
Kubenea
amesema kuwa ukumbi ulikuwa mdogo na walitakiwa kuthibitisha ushiriki,
hivyo ukumbi usingeweza kujaza wabunge wote wa CHADEMA na Dar es salaam
hayuko yeye peke yake.
“Naweza
shiriki uzinduzi saa nne asubuhi na mchana nikahama, kwahiyo
nisihukumiwe kwa kutoshiriki kwangu, kwakuwa haikuwa lazima na hakuna
uhusiano wowote baina ya sera na kuhama, na sikuwa peke yangu Dar es
salaam tuko zaidi ya saba”, amesema Kubenea.
Septemba
25, 2018 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilizindua kitabu
cha sera za chama hicho toleo la mwaka 2018 kikiwa na sera 12 ambazo
zimezungumzia namna ambavyo chama hicho kimejipanga kuinua maisha ya
mtanzania, suala lililoibua maswali ni kwanini Mbunge wa Ubungo Saed
Kubenea hajaonekana katika eneo la tukio bila kuwa na taarifa kwa Umma.
Mbali
na hilo Kubenea pia amekuwa nyuma katika majukwaa ya CHADEMA ikiwemo
kutoonekana ushiriki wake katika kampeni za uchaguzi mdogo wa majimbo ya
Ukonga na Monduli, baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa wabunge walioko
mbioni kutimkia CCM kutokana na kutokuwa na maelewano na mwenyekiti wa
chama hicho taifa, Freeman Mbowe, tuhuma ambazo yeye amekuwa akizikataa
na kudai hakuna wa kumuondoa.
Post a Comment