UWT ILALA YATOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani , Umoja wa Wanawake wa Chama chaMapinduzi (UWT) Wilaya ya Ilala wameendelea kufanya kazi za kujitolea katika jamii na kutoa misaada ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali ambapo leo wamefanya kazi hizo katika hospitali ya Mama na mtoto chanika.
Akizungumza Hospitalini hapo mara baada ya wanawake hao kufanya kazi ya usafi na kutoa msaada katika wodi za wazazi , mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Amina Dodi , amewataka wanawake kutojiweka nyuma katika shughuli za maendeo na kugombea Nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kuwaachia wanaume pekee .
‘’Dodi amesema ,wanawake wana wajibu wa kugombea nyazifa zozote za uongozi zinapotangazwa wawe mstari wa mbeĺe katika kugombea wasiwe nyuma’’amesema
"Wanawake wa Wilaya ya Ilala leo tumeungana na wanawake wote katika siku hii ya wiki ya Wanawake wa CCM kuanzia O ktoba Mosi hadi Octobar 3 tukishiriki usafi na kazi za kijamii" amesema.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT Wilaya ya Ilala Batuli Mbaraka Mziya, ameipongeza Serikali kwa kuwajali wanawake na kuwajengea hospital ya Mama na mtoto, na kuwataka wanawake wanapo adhimisha sikuhiyo kupendana na kusaidiana.
‘’ Naipongeza Serikaĺi ya awamu ya tano na Rais John Magufuli kwa kujenga hospitali ya Mama na Mtoto hapa kata ya Chanika ni jambo jema wanawake kwa sasa wanajifungua karibu na eneo lao hawasumbuki tena kufuata huduma hizi Amana” amesema
Naye Diwani wa Viti Maalumu Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo, aliwataka wanawake wa Wilaya ya Ilala kuchangamkia fursa za kiuchumi na mikopo inayotolewa na serikali ili kujiendeleza kibiashara na kuinua kipato chao .
Kanansia Michael Shoo , ni Daktari kiongozi wa Hospitali hiyo akitoa neno la shukrani amewashukuru wanake wa UWT Ilala kwa moyo wao wa kujali na kuyataka makundi mengine kuwa na moyo huo.
Siku ya wanawake duniani kwa wana ccm , huadhimishwa kila mwaka ifikakapopo tarehe Mosi hadi 3 Oktoba , ambapo wanakewa huzitumia siku hizo kufanya shughuli za kujitolea katika jamii.
Post a Comment