Ads

BALOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA AZINDUA FILAMU YA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI

Mwamba wa habari
Kwa sera ya elimu bure serikali inatakiwa kupongezwa sana, lakini pia nguvu kubwa inatakiwa kuwekwa katika elimu ya stadi za maisha kwa watoto wakike ili waweze kujitambua na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Balozi wa Sweden nchini Bw, Anders Sjoberg (katikati) akizindua filamu inayoonyesha madhara ya ndoa za utotoni na kulia kwake ni Mkurugenzi wa (CDF) Koshuma Mtengeti  na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID).

Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Bw. Koshuma Mtengeti katika siku ya pili ya Kongamano la Sauti za Wasichana lililofanyika katika chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).

Kongamano hilo limefungwa rasmi siku ya jana tarehe 10 mwezi huu wa 10 na Balozi wa Sweden hapa nchini ambapo pia amezindua filamu fupi ya kuonyesha mapungufu ya sharia yetu ya ndoa inayotoa idhini kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka chini ya 18 wakati kwa mtoto wa kiume inakubali kuoa akiwa na umri stahiki wa miaka 18.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa wamekaa kwa muda wa siku mbili na wasichana hao kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwapa maarifa mbalimbali kuhusiana na Elimu ya afya ya uzazi, namna ya kujitambua na jinsi ya kukabiliana na changamoto za kimaisha ikiwa ni pamoja na mimba za utotoni.

Aliendelea kusema kuwa ni vema katika harakati hizi wakahusishwa wazee wa kimila pamoja na viongozi wa kidini, kwani wao ni watu wanaosikilizwa sana katika jamii na pia wananguvu kubwa ya kuleta mabadiliko, ili Tanzania iwe ni nchi yenye wanawake na watoto wanaofurahia haki zao na waweze kuchangia katika uchumi wa nchi yao.

Kwa upande wake balozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Anders Sjoberg alisema kuwa wao kama nchi huru wameweka nguvu kubwa katika usawa wa kijinsia kwa kuthamini makundi yote wanawake kwa wanaume kuwa na usawa katika rasilimali na hata katika ngazi za maamuzi na uwakilishi.

Aliendelea kusema kuwa wao pia wemewekeza katika elimu kuanzia shule za msingi, sekondary mpaka chuo kikuu kwa kuhakikisha watoto wote wakike kwa wakiume wanapata elimu bora, vivyo hiyo watashirikiana na Tanzania katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama na kupata haki zao stahiki.

Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg akiongea na waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya waandishi wa habari katika Kongamano la Sauti za Wasichana mapema jana jijini Dar es saalaam.


 Meza kuu ikiwa katika safu yake.


Afisa habari wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Michael Jackson Sungusia akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mbele ya Mgeni Rasmi.


Wasichana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakifuatilia Kongamano kwa umakini.

No comments