CRDB yataja washindi wawili wa wiki wa Shindano la Shinda na SimAccount
Na.Hussein
Ndubikile,
Mwambawahabari
Washindi
wawili wamejipatia kitita cha Sh.Mil 3 kupitia Shindano la Shinda na SimAccount linaloendeshwa na Benki ya CRDB
ambapo benki hiyo huchezesha droo ya shindano hilo na kuwataja washindi.
Akichezesha
droo hiyo mbele ya wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa benki
hiyo, Ariel Mkony alimtangaza mshindi wa kwanza aliyepatikana kutoka mkoani
Lindi aliyejitambulisha kwa jina la Cuthbert Mwakatumbula(34) ambaye pia ni
askari Magereza aliyeshinda fedha taslimu Sh.Mil 2.
Amesema
tangu waanze kuchezesha shindano hilo wamekuwa na utaratibu wa kuwataja
washindi wa wiki na mwezi ambapo hujinyakulia fedha taslimu kwa kujisajili
katika huduma ya SimAccount.
“Shindano
linaendelea vizuri tunawaomba wananchi waendelee kucheza kwa kujiunga na huduma
ya SimAccount itayowafanya wateja
wajikwamue kiuchumi,”amesema Ariel.
Kwa upande
wake,Mshindi, Cuthbert amesema amepokea kwa furaha zawadi hiyo na kwamba
imemuaminisha kuwa shindano hilo halina upendeleo.
Naye, Adela
Kaliseni (40) mshindi kutoka wilayani Korogwe, Tanga amepokea taarifa ya
ushindi wa kitita cha Sh. Mil 1 huku haamini na kusisitiza ataamini mpaka atapoingiziwa
fedha zake kwenye akaunti yake.
Kaliseni
ambaye ni Askari Magereza mkoani humo amebainisha fedha hizo atazitumia
kuongeza ng’ombe wa kisasa wa maziwa.
Benki yaCRDB
kupitia Meneja huyo imesema mpaka jumla ya washindi 684 wamejishindia fedha
taslimu tangu kuanzishwa kwa shindano hilo huku washindi 648 wakijishindia
fedha taslimu Sh 5,000, Sh 20,000 katika
nyakati za asubuhi na jioni .
Ameongeza
kuwa hadi sasa washindi wa kila wiki 36 wamejishindia fedha taslimu Sh mil 2 na Sh Mil 1 na Kubainisha wiki ijayo
watachezesha droo ya mwezi ya Sh Mil.10.
“ Mteja hana
haja kwenda kwenye tawi la benki au wakala kupanga foleni bali anaweza kujiunga
kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*62 # , akiwa na kitambulisho cha
kupigia kura anaingiza namba zilizomo kwenye kitambulisho’” amesema.
Balozi wa
SimAccount, Zena Mohamed ‘Shilole’ amewataka wananchi kushiriki shindano hilo
kwani litawasiadia kujikwamua kiuchumi.


Post a Comment