Ads

RC TABORA : WAKULIMA NA WAFUGAJI ENDELEZENI SHUGHULI KISASA ZITAKAZO CHOCHEA UANZISHAJI WA VIWANDA.

Mwambawahabari
NA TIGANYA VINCENT
RS Tabora
22 SEPTEMBA 2018
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka wakulima na wafugaji mkoani humo kuendesha shughuli zao kisasa ili waweze kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitachochoa uanzishaji wa viwanda katika eneo hilo.
Alisema anaweza kujenga Kiwanda katika eneo ambalo hana uhakika  malighafi za kutosha wakati wote kwa ajili ya uzalishaji bidhaa mbalimbali.
Mwanri alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifungua  warsha ya utetezi majadiliano  katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji iliyowahusisha viongozi wa Serikali na sekta binafsi mkoani hapa.
Alisema kuwa ili Tabora iweze kupata maendeleo  kupita Viwanda  wakulima na wafugaji wanaowajibu wa kuzalisha malighafi nyingi kwa kuachana na kilimo cha kizamani na ufugaji wa mifugo ambayo haizalishi nyama nyingi na maziwa mengi.
“Yupo rafiki yangu mmoja aliniambia Mkuu wa Mkoa muombe  AZAM aje afungue Kiwanda cha Matunda hapa Tabora kwa kuwa tunayo miembe mingi …ni kwambia ili kiwanda kifunguliwe ni lazima Mwekezaji awe na uhakika wa kupata maembe kutosha mwaka mzima…tukitaka tufanikiwa hilo ni lazima tuanze kilimo cha miembe ya kisasa ambayo inazalisha maembe ambayo yanamwezesha kupata matunda ya kutosha kuendesha kiwanda mwaka mzima” alisema.
Mwanri alisema ni vema wakazi wa Tabora wakatumia fursa zilizopo za kufunguka kwa barabara na miundombinu mbalimbali iliyopo kujikita katika kilimo cha kisasa na uzalishaji wenye tija kwa ajili ya maendeleo yao.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema endapo fursa zilizopo hazitatumiwa vizuri wananchi wasitegemee maendeleo bali watabaki watazamaji.
Aliziagiza Halimashauri zote kuhakikisha zinapima na kutenga maeneo na kuweka miundombinu kwa ajili ya wawekezaji ambayo itawafanya wasipate shida pindi wanapotaka kuwekeza.

Aidha Mwanri aliwaasa wafanyabiashara kuwa wabunifu na kuingiza bidhaa mpya ambazo hazina ushindani mkubwa kwa kupenda kuendesha bidha za aina moja katika eneo moja na kusababisha mzunguko kuwa mdogo wa fedha kwa sababu ya kugawana wateja.

No comments