BARAZA KUU CUF WAKUTANA KUJADILI AJENDA ZITO I2.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF) wakiwa katika Mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baraza Kuu la Uongozi Chama cha Wananchi (CUF) wamekutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili ajenda zisizopungua I2 zenye lengo kuangalia mustakabali wa Taifa la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa kikao hicho cha Baraza kuu kitafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo.
Profesa Lipumba amesema kuwa Baraza litajadili ajenda zisizopungua I2 ambazo zote zimelenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa haki na furaha kwa watanzania.
"Tutajadili matatizo tuliyonayo jambo ambalo litasaidia kupiga hatua za kimaendeleoa katika nchi yetu" amesema Profesa Lipumba.

Post a Comment