Ads

Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.

 
 
 
Na Mwandishi Wetu
mwamba wa habari
Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza limeanza ziara
ya kutoa elimu juu ya ugonjwa huo katika mikoa ya Kanda
ya Ziwa. 
 
Hayo yamesemwa leo na  Meneja Mradi wa Shirikisho hilo Happy 
Nchimbi,ambapo amebainisha kuwa tayari wameanza kampeni inayolengo 
kuvifikia vyuovya mbali mbali nchini  na shule za msingi na sekondari 
kuelimisha juu ya ugonjwa huo.

Amesema  kuwa shinikizo la juu la damu ni kati ya magonjwa 
yasiyokuwa ya kuambukizwa ambapo asilimia ya wagonjwa wa 
ugonjwa huo haioneshi kupungua.

"Tumeanza kampeni hiyo katika mikoa ya kana ya ziwa ambapo
kuanzia septemba 20 na 21 tumetoa elimu juu ya magonjwa hayo
kwenye Chuo cha Walimu Shinyanga na kuwa zoezi la uelimishaji
limepokelewa vema,"amesema Happy.

Happy amesema kuwa zoezi hilo linaendelea septemba ambapo
Septemba 22 na 23 watakuwa Chuo cha Walimu Butimba mkoani
mwanza.
 

Amesema katika kuendelea na uelimishaji huo Kanda ya Ziwa Septemba
24 na 25 watakuwa Musoma Utalii Teachers and High School .

Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza limeanza ziara hiyo 
ikiwa ni kuhakikisha vijana wanapata elimu ya kutosha ili kuweza
kuelimisha UMMA na familia zinazozingatia mitindo bora ya maisha
ikiwa pamoja na ulaji unaofaa na kufanya mazoezi na kuepuka 
matumizi ya Sigara na unywaji wa pombe uliozidi.


Meneja huyo pia alisisitiza kuwa kwakuwa serikali ina mpango 
wa kurekebisha mitaala ya elimu nchini Shirikisho hilo la Magonjwa 
yasiyo ya Kuambukiza limeanza kampeni kutaka magonjwa yasiyo 
yakuambukizwa kuingizwa katika mitaala.

 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo yakuambukizwa Profesa Andrew
Swai alisema  kampeni waliyoianzisha ya kupima kwa hiari magonjwa ya 
kuambukizwa iliyoamzia katika viunga vya Chuo Kikuu Huria Dar es Salaa
Salaam hivi karibuni alisema tatizo kubwa lipo katika ulaji usiofaa,kwakuwa watu
wamekiuka misingi ya ulaji usiofaa na badala yake hujilia kwa kadri wawezavyo
hivyo ameitaka jamii kuzingatia ulaji unaofaa.


Profesa Swai alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la Afya duniani 
za mwaka 2012 na tafiti zinazofanywa marakwamara na Shirikisho la Vyama vya
Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza, inaonesha shinikizo la juu la damu ni ugonjwa 
unaongoza kuliko magonjwa yote yasiyo kuwa ya kuambukizwa.

Ripoti ya ya WHO ya 2012 inaonesha wagonjwa wanaougua plesha wanaongoza kwa 
aslimia 26, sukari asilimia 9, na hata baada ya utafiti huo imeonekana ugonjwa 
wa plesha umeongezeka mara tatu kuanzia 2012.


Imeelezwa kuwa watu 9 kwa kila 100 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25
na kuendele wana ugonjwa wa kisukari,hata hivyo inatajwa kuwa kati ya 
hao 9 ni wawili tu wanaojijua kuwa wanakisukari.

No comments