(JKCI) KUFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO BILA MALIPO KATIKA VIWANJA VYA HOSPITALI YA VIJIBWENI WILAYANI KIGAMBONI
Mwambawahabari 
TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA
MOYO DUNIANI
TAREHE 29/09/2018
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda
kuwajulisha wananchi kwamba itafanya
upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo katika Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni
jijini Dar es Salaam. Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia
saa 2 (mbili) asubuhi. Wananchi wote mnakaribishwa.
Kauli mbiu: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote
pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.
Limetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete
27/09/2018
Post a Comment