MIRADI YA AFYA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI UZINGATIE THAMANI YA FEDHA.
Na
Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR
ES SALAAM
SERIKALI
imeendelea kutoa kipaumbele katika huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia
wananchi wote ili kuboresha afya zao kwa kutambua kuwa afya bora ni raslimali
muhimu kwa maendeleo.
Maendeleo
ya Taifa lolote la duniani yanaletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa
kuzalisha mali na Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa
huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.
Kabla
ya Uhuru, huduma za afya nchini zilikuwa zinatolewa zaidi kwenye maeneo ya
shughuli za kiuchumi kama miji na mashamba makubwa na baada ya Serikali iliweka
msukumo zaidi katika kupanua huduma za afya ili kuwafikia wananchi wengi hasa
walioko vijijini.
Ili
kufanikisha azma hii, Serikali iliweka mfumo wa rufaa wa huduma za afya kupitia
mfumo wa zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, hospitali za mikoa,
maalum, kanda na taifa zilianzishwa.
Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kuimarisha na
kuboresha huduma katika sekta ya afya
kuanzia katika ngazi ya kijiji mpaka Hospitali ya Taifa.
Moja ya mipango ya
haraka inayotarajiwa kufanikishwa kwa ufanisi mkubwa na Serikali ni pamoja na
kuimarisha miundombinu na mahitaji ya watumishi wa kada za afya kuanzia ngazi
ya zahanati, vituo vya afya, hospitali ya wilaya na hospitali ya rufaa ya mkoa.
Katika bajeti ya
Mwaka 2018/19, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
imeliomba Bunge kuiidhinisha kiasi cha Tsh Trilioni 1,458,291,418,500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, maji, elimu, barabara n.k
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mwaka 2018/19,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jafo anasema Serikali
imeongeza bajeti ya dawa, vifaa, vifaa tiba, chanjo na vitendanishi kutoka Tsh.
Bilioni 31 zilizotengwa Mwaka 2015/16 hadi Tsh. Bilioni 269 zilizotengwa katika Mwaka 2017/18.
Anaongeza kuwa katika
ya fedha hizo, Tsh. Bilioni 98.08
zimetengwa kwa ajili ya huduma ya afya ya msingi kwenye Hospitali za Wilaya,
Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na ongezeko la upatikanaji wa dawa muhimu kufikia
asilimia 92 ikilinganishwa
na asilimia 81 katika kipindi
kama hicho Mwaka 2016.
Aidha Waziri Jafo
anasema Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya 208 ili kuviwezesha kutoa huduma za
dharura za upasuaji kwa ajili ya kuboresha huduma zote za Vituo vya Afya. Kati
ya Vituo hivyo 15 ni vipya na 14 ni zahanati zilizopandishwa hadhi
na vituo vitatu (3) ni maboma yasiyokamilika.
“Vituo vya Afya
vilivyopo ni 696 sawa na
asilimia 15.7 ya lengo la kuwa
na Vituo vya Afya 4,420 ambapo kati
ya hivyo, vituo 513 vinamilikiwa na Serikali na vituo 183 vinamilikiwa na Sekta Binafsi
na Mashirika ya Dini” anasema Waziri Jafo.
Akifafanua zaidi
Waziri Jafo anasema ujenzi wa vituo hivyo utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni
93.5 hadi kukamilika kwake pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 50.2 kwa ajili ya
kununulia vifaa tiba pamoja na samani ili kuviwezesha kuanza kutoa huduma.
Anaongeza kuwa Ofisi
yake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto zimeandaa mkakati wa pamoja wa kukamilisha ukarabati na ujenzi wa vituo
vyote ili kuboresha huduma za Afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi
kupitia wadau wa maendeleo wa Mfuko wa Pamoja wa Afya.
Sanjari na ujenzi wa
vituo vya afya, Waziri Jafo anasema katika mwaka 2017/18 Serikali
iliidhinishiwa na Bunge Tukufu jumla ya Tsh.
Bilioni 35.5 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Zahanati, kipaumbele
kikiwa ni kukamilisha ujenzi wa maboma yaliyoanza kujengwa kwa nguvu za
wananchi.
“Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekamilisha ujenzi wa nyumba 578 za watumishi wa afya
katika vituo vya afya 268
kwenye Halmashauri 51, lengo
ni kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za Afya kinakuwa na nyumba angalau
mbili ifikapo Mwaka 2020 ili kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi” anasema
Waziri Jafo.
Waziri Jafo anasema
Ofisi yake pia imeanza matumizi ya mfumo wa jazia kwa kutumia Washitiri (Prime
Vendor) katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Shinyanga ambao lengo ni
kuhakikisha dawa zinakuwepo katika vituo vya kutolea huduma za Afya endapo
zimekosekana katika Bohari Kuu ya Madawa.
Anaongeza kuwa azma
ya Serikali ni kuhakikisha mfumo huu unatumika katika Mikoa yote 26 nchini.
Ili kufanikisha azma
ya Serikali kufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda ifikapo mwaka
2025, ni dhahiri kuwa afya ndiyo mtaji na msingi mkuu wa mafanikio hayo katika
uzalishaji mali katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Post a Comment