Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani wafanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto 23
Mwambawahabari
Madaktari bingwa wa
magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
kushirikiana na wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini
Marekani wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo kwa kutumia
mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya matibabu ya siku tatu iliyomalizika
jana. Upasuaji huo hufanyika bila kufungua kifua kwa kupitia tundu dogo
linalotobolewa kwenye paja. Jumla ya watoto 14 wenye matatizo ya moyo ya
kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa kuziba matundu
na kutanua mishipa ambayo haipitishi damu vizuri na hali zao zinaendelea vizuri.
Madaktari bingwa wa upasuaji
wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na
wenzao wa Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanya mtoto
upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefanyiwa
upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na Genofeva Matemu – JKCI

Post a Comment