MEYA KUYEKO, AFURAHISHWA NA KAZI YA MASHAMBA DARASA YA ILALA NANENANE MOROGORO.
Mwambawahabari
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Charles Kuyeko amewapongeza Wakulima na wadau wa Kilimo wa Manispaa ya
Ilala kwa kazinzuri waliyoifanya katika shamba darasa la Manispaa hiyo lililopo
hapa mjini Morogoro katika viwanja vya nanenane.
Kuyeko ameyasema hayo baada ya
kutembelea shamba darasa la Manispaa hiyo ambapo amejiionea shughuli za
Wakulima , wafugaji na Wajasiliamali wa mazao ya kilimo na Mifugo
wanaoshiriki maonesho wa Wakulima katika viwanja vya nanenane mjini hapa.Amesema, Nanenane ya mwakahuu imekuwa bora na kueleza kufurahishwa kwake na kilimo cha Uwiano kinatumia mazingira, na kilimo cha mbogamboga na mazao mengine na kusema kuwa kunatija katiki kushiriki maonyesho hayo ukilinganisha na miaka iliyopita.
Kwa upande wa ufugaji wanaonea namna ya kufunga samaki, kuku, bata, Sungura ng'ombe na mbuzi.
Post a Comment