AF, FDT, YATAMBULISHA FURSA YA UWEKEZAJI SEKTA YA MISITU.
Mkurugenzi waTaasisi ya Ki-uanachama ya African Forestry (AF) Francis Rwebogora akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha Mtandao wa MITIBIASHARA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.Taasisi ya Ki-uanachama ya African Forestry (AF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Uendeshaji Misitu (FDT) wametambulisha Jukwaa la kuwasaidia wawekezaji katika sekta ya kilimo cha misitu jambo ambalo litasaidia uzalishaji malighafi.
Jukwaa hilo limelenga kutoa elimu ya kilimo cha miti kwa njia ya Mtandao kupitia App ya 'MITIBIASHARA' jambo ambalo litasaidia kufanikisha Tanzania ya Viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Taasisi ya Ki-uanachama ya African Forestry (AF) Francis Rwebogora, amesema kuwa miti ni zao muhimu katika sekta ya ujenzi, viwanda pamoja na kutengeneza samani.
Amesema kuwa kutokana na umuhimu wa misitu wameona ni vyema kutoa elimu juu ya biashara ya miti ili kuhakikisha kila mtu ananufaika na uwekezaji wa miti.
Rwebogora amesema kuwa ni wakati umefika watanzania kujiunga na Jukwaa hilo ili kukutana na wadau mbalimbali katika sekta ya Misitu, ikiwemo wakulima wa miti, wafanyabiashara, makapuni makubwa ya misitu pamoja na watafiti.
"Kuna ukosefu wa taarifa sahihi zinazohusu kilimo cha miti, kuanzia kuandaa shamba, upatikanaji wa mbegu bora, utunzaji wa shamba, masoko, pamoja na ushauri wa kitaalamu"amesema Rwebogora.
Mwezeshaji wa Biashara katika Taasisi hiyo Emmanuel Sangalali, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wawekezaji katika Kilimo cha miti wanapata taarifa sahihi ikiwemo mafunzo stahiki kupitia Jukwaa Maalum.
Amesema kuwa Jukwaa hilo limesheni taarifa na mijadala yenye lengo la kuwawezesha wawekezaji kuwekeza wakiwa na uwakika bila kupoteza fedha.



Post a Comment