Ads

Manispaa ya Ilala yatoa ushauri nasaha bure nanenane Morogoro





Wakulima wa KIPUNGUNI wakiwa shamba banda la nanenane Morogoro Leo (Picha na Heri Shaban)
Na Heri Shaban,Morogoro


Muuguzi kiongozi wa Magonjwa ya nje MANISPAA ya Ilala Johari Yusuph akiangalia mahindi katika shamba la Manispaa ya Ilala viwanja vya wakulima Nanenane Morogoro leo,(kulia) Dkt Angelina Minja (PICHA NA HERI SHAABAN)


MANISPAA ya Ilala imewaomba wananchi wa Manispaa ya morogoro na mikoa Jirani  kufika katika banda la manispaa ya Ilala kwa ajili ya kupatiwa huduma za ushauri nasaha na huduma ya kwanza bure.

Hayo yalisemwa Mkoani Morogoro Jana na Muuguzi Kiongozi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja  Johari Yusuph, ambaye anatoa huduma ya ushauri nasaha, huduma ya kwanza
bure katika banda la Ilala morogoro.

"Tumeshiriki wiki ya maonyesho ya Wakulima nanenane katika banda letu la Manispaa Ilala kila mwaka tumeweka taratibu wa kutoa huduma ya kwanza,kupima Vvu, Kisukari, ushauri nasaha bure hivyo tunawaomba wananchi wafike katika letu,kwa ajili ya kuangalia afya Zao.

Johari aliwata wananchi kujenga taratibu wa kuangalia afya zao kila wakati katika vituo vya afya Serikali kinga ni bora kuliko tiba.

 Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Estar Msome, amewataka wananchi kufika katika banda la Manispaa ya Ilala kujifunza kilimo cha kisasa,kilimo cha Magorofani, kilimo cha uwiano.

Masome alisema katika manispaa hiyo ukifika utajifunza njia mbalimbali za Kilimo ikiwemo utunzaji wa mazao baada ya mavuno.


Pia Manispaa hiyo utajifunza usindikaji mazao mbalimbali  ,kilimo cha uyoga na uchakataji maji taka.

Kwa upande wake Dkt. wa Mifugo manispaa hiyo, Jawb Mwasha alisema kwa Maendeleo ya ufugaji Tanzania ni muhimu kwa wafugaji kutambua muda gani hasa ng'ombe alianza kunyonyesha dalili za joto ili kumwezesha mtaalam kupanga mda mzuri.

Mwasha alisema ili kulinda mifugo yako kutokana na magonjwa ya kizazi yanayosambazwa na madume baaadhi usababisha ugumba na utupaji wa mimba.

Alisema baadhi ya magonjwa ya mifugo ya ng'ombe yanayosambazwa na ng'ombe dume usababisha magonjwa kwa binadamu.

No comments