ZIARA ARUSHA NA MERU DC Jerry Murro
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro Leo amefanya ziara ya kikazi pamoja utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri Mbili za Meru DC yenye kata 26 na Arusha DC yenye kata 27 zilizo katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Akiwa katika Halmashauri Hizo amewataka watumishi kufanya kazi kwa Kuzingatia Mahitaji ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambayo ndio anasimamia Utekelezaji wake katika Halmashauri zote Mbili Zenye kata 53*
Katika Ziara Hiyo Mhe Muro ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe Iddi Hassan Kimanta* aliekuwa akikaimu Wilaya ya Arumeru, pamoja na Katibu tawala Bwana *Timotheo Mzava pamoja na baadhi ya Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Arumeru.


Post a Comment