JAFO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI KIMBIJI KUTOA POLEA KUFUATIA KIFO CHA WANAFUNZI WANNE.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo amewataka walimu na wakuu wa shule zote nchini kutowaruhusu wanafunzi kufanyia sherehe katika maeneo mageni wasiyo yazoea ili kuwalinda na ajali zinazoweza kuwa kuta.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo amewataka walimu na wakuu wa shule zote nchini kutowaruhusu wanafunzi kufanyia sherehe katika maeneo mageni wasiyo yazoea ili kuwalinda na ajali zinazoweza kuwa kuta.
Waziri Jafo Ameyasema hayo leo alipofika kutoa pole katika
shule ya sekondari Kimbiji Manispaa ya Kigamboni kufuatia vifo vya
wanafunzi wanne walikufamaji juzi tarehe 28,walipokuwa wakiogelea bahari
ya Hindi wakiwa katika sherehe ya kujipongeze baada ya shule yao
kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na kumi bora katika mkoa katika
mtihani wa MOCK.
Amesema agizo hilo amelitoa kwakuwa kunamatukio mengi
yamekuwa yakiripotiwa na kufanyahivyo kutasaidia kupunguza na kukomesha
matukio hayo, na kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili na kuwatia moyo
kwa msiba mkubwa uliowapata .
"Wanafunzi mnatakiwa sasa kuwa nasubira kwa kipindi hiki
kigumu maana ninyi sasa ni familia moja hapa shuleni akitutoka
hatammojatu kati yenu unakuwa ni msiba kwetu sote, Mwenyezi Mungu
atawafanyia wepesi mtafaulu mitihani yenu lakini piamsisahau kuwaombea
wenzenuwaliotanguliambele ya haki Mwenyezi Mungu awaandalie mazingira
mazuri " alisema
" Zamani tulikuwa na walimu wachache lakini kwa sasa
nimeambiwa mna walimu zaidi ya 20,tumienifursahii vizuri kuwa sumbua
walimu wenu wawafundishe kile ambacho wanacho .
Hatahivyo amesema kuwa serikali inatoa shilingi bilioni 23.8kila mwezi kugharamia Elimubure ili wanafunzi waweze kusoma.
Pamoja na hayo Jafo amesema Ofisi yake kupitia Katibu Tawala wa
Wilaya ya Kigamboni itafikisha ujumbe wa ofisi ya Rais na rambirambi
pamoja kuwajulia hali wafiwa wote.
Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Raheli
Mando , amemshukuru Waziri Jafo kwa kufika shuleni hapo na kuahidi
kuyafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa .




Post a Comment