Na Muandishi Wetu
Mwamba wa habari
Benki kongwe
ya kibiashara nchini Tanzania KCB imetoa kiasi cha shilingi million 420
kudhamini ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania Bara(VPL) kwa msimu wa mwaka
2018/2019.
Akiongea na
waandishi wa habari katika makabidhiano ya hundi hiyo mapema leo jijini Dar es
salaam Mkurugenzi Mtendaji wa KCB benki Bw. Cosmas Kimario alisema kuwa hii ni
mara ya pili kwa KCB kudhamini mashindano hayo.
“Hii ni
mara ya pili tunakutana katika hoteli hii ya Serena kwa kuwa tulishakaa kikao
kama hiki kwa mwaka jana kati ya KCB Benki na chama cha Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kwa lengo kama hili la kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara”.
Alisema Kimario
Katika udhamini huo KCB Bank imeongeza
thamani ya udhamini wake katika ligi hiyo kutoka kiasi cha shilingi za
Kitanzania 325,000,000 msimu wa 2017/18 mpaka shilingi 420,000,000 msimu wa
2018/19 huku ongezeko likiwa ni ziadi ya milioni 90,000,000,
Aliongezea kuwa
benki ya KCB ina nia thabiti ya kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini na ndio
maana imeamua kuwekeza katika ligi kuu Tanzania bara, lakini pia inaangalia
uwezekano wa kuendelea kudhamini ligi nyingine kama ligi daraja ya kwanza na
nyinginezo.
Kwa upande
wake Rais wa TFF Wallace Karia alisema kuwa tusiwe na utaratibu wa kuziogopa
benki kwani mabenki yana pesa nyingi ambazo zinahitaji watu wanaoweza
kuzitengenezea njia nzuri ili ziweze kujizalisha na kuleta faida kwao na kwetu
sisi tunaopewa udhamini.
Aliendelea kusema
kuwa kama tulivyoshirikiana vizuri kwa mwaka jana hivyo hivyo tutaonyesha
ushirikiano mzuri kwa mwaka huu kwa benki ya KCB kwa kuwa ni watu ambao wapo karibu
sana na sisi na ni watu wanaozijua vizuri shida zetu.
Kaimu
Menyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi. Fatma Chillo alisema kuwa ni fursa
ya kipekee kuweza kudhamini Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili. “Lengo
letu ni kuleta hamasa kwa timu na mashabiki wa mpira wa miguu kwa kuzijengea
timu, hata zile ndogo uwezo wa kifedha ili kuziwezesha kushindana kikamilifu
hivyo kuongeza ushindani ndani ya ligi.” Alieleza Bi. Chillo.
Rais
wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru KCB Bank Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu
Vodacom jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu
2018/19. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza
kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi
kuu.
Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia Akiongea na waandishi wa habari leo Serena hotel jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Benki Tanzania Bw. Cosmas Kimario akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Bw. Wallace Karia wakikabidhiana mkataba baada ya kusaini Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni 420 .
Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wa KCB Benki na TFF baada ya Tafrija kuisha.
Post a Comment