"WANA WAKE WAWEZESHWE KUFANYA BIASHARA NA MIRADI MIKUBWA SIYO BATIKI NA UREMBO PEKEE" DC MJEMA.
Mwambawahabari
Mlezi wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala mhe. Sophia Mjema amelitaka Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi JUWADA kuwa fundisha wanawake kuwa serikali inayo mifuko 19 ya kuwa wezesha kiuchumi ambayo wanaweza kuitumia ili kujiendeleza kibiashara.
Mjema Ameyasema sema hayo katika mkutano wa semina ya Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam iyofanyika Mlimani City, na kuongeza kuwa wanawake wanao uwezo mkubwa wa kuendesha biashara kubwa na uwekezaji katika Kilimo, Madini na Uvuvi ikiwa watawezeshwa kupata mitaji.
"Wanawake hawa wanataka kuwezeshwa ndiyo maana wako hapa Katibu wangu naomba muwafundishe kuwa serikali ya awamu ya tano inayo mifuko 19,wawezesheni kwenye mifuko ya kilimo, Bara Bara, hata uvuvi mwanamke anwezakumwajiri mtu na aka fanya shughuli za uvuvi, tusiwaachie wanaume tuhizi kazi hizi wanawake tuna weza"Amesema
Aidha amesema imefika wakati wanawake kufanya biashara na miradi mikubwa na sikila wakati Wana an zishatengwa biashara la batiki, na Sabuni tu.
"Tunataka wanawake watakao kuwa kama Maida, wajenzi wa mabarabara na taifa hili lita piga hatua kubwa ikiwa wanawake tutawawezesha na wasiwe tegemezi kwa Wanaume tu hii ndiyo dhamana ya Kiongozi wetu aliye anzisha majukwaa haya Mama Samia Suluhu" Amesema.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika Mkutano huo ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda biashara, na uwekezaji Mhe. Stella Manyanya amewataka wanawake kutumia fursa zilizotolewa na serikali, mikopo na Elimu ya ujasiriamali mali inayo tolewa ilikujiendeza kiuchumi.
Hata hivyo ametoa wito kwa Wanawake hao wajasiriamali kupata elimu ya kutosha na kuona umuhimu na kujiunga kupata nembo za Simbo milia ambazo zita wa tambulisha katika biashara kitaifa na kimataifa.
"Natoa agizo tunakaribia kuanza maonesho ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya saba saba Mkurugenzi ahakikishe anaendeakutenga nafasi za kutosha kwa wajasiriamali wa ndani. Amesema.
Post a Comment