Ads

CDF KUINOA KAMATI YA KUPINGA UKATILI WA MTOTO



Mwambawahabari
JUKWAA la utu wa mtoto  (CDF ) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam limeandaa mafunzo maalumu  ya siku tatu kwa Kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto katika kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,Mapema Leo hii, Mwakilishi wa Jukwaa hilo, Yared Bagambilana amesema kuwa, mafunzo hayo yamelenga kutekeleza mpango wa kitaifa  (MTAKUWWA) wa miaka miatano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha amesema kuwa,wameamua kufanya mafunzo hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Viongozi wa dini pamoja na Asasi za kiraia ikiwa muendelezo wa program na mipango mbalimbali ambayo imelenga kukuza, kutetea na kuboresha haki na ustawi wa mtoto katika jamii kwa kupinga ukatili wa kijinsia.

Amesema kuwa, ukatili wa kijinsia bado upo kwa badhi ya mikoa ingawaje wanafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanautokomeza ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam wanafanya kazi zaidi katika kata ya kitunda kwani inaonekana bado waendelea na tamaduni kutoka katika mikoa yao jambo ambalo ni kinyume cha sheria pamoja na kukiuka haki za mtoto.

Ameongeza kuwa, katika mafunzo hayo wameamua kushirikisha wadau mbalimbali ambapo wanaamini watakua ni mabalozi wazuri wa kutoa elimu katika jamii kutokana na wao wa nakutana na watu wengi hivyo, wanatumia fursa hiyo kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto na mwanamke.

Kwa upande wake, Afisa ustawi wa Jamii mkoa wa Dar es Salaam  Flora Masuya amesema kuwa, Serikali imekua ikitumia fedha nyingi katika kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia , hivyo ni vyema kila mtu kwa nafasi akawa balozi wa kutoa elimu ili kuhakikisha tatizo hilo linaondoka.

Aidha amesema ,katika suala la ukatili wa kijinsia bado lipo kutokana na kuwa watu hawaelewi maana ya ukatili,kwa mfano katika mkoa wangu wanaume asilimia kubwa hawana elimu ya ukatili wa kijinsia ndio maana tunapokea ripoti ndogo sana ikilinganishwa na wanawake.

Ameongeza kuwa, kupitia mafunzo hayo anaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa pamoja na kujua aina za ukatili na hatua gani za kuzichukua pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili wa aina yoyote katika jamii.

No comments