Ads

ZOEZI LA USAFI ILALA, MPOGOLO AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUTOTUPA TAKA HOVYO.

 Mwambawahabari 
Ikiwa leo ni siku ya usafi wa mazingira ambayo unafanyika kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wamefanya usafi katika daraja la Salenda  pamoja na Pembezoni mwa  Ufukwe  wa eneo hilo kutokana na taka nyingi zilizotoka katika mto msimbazi.
 Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ilala katibu tawala wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo amesema leo wameamua kufanya usafi katika eneo hilo  la  Salenda lengo likiwa ni kuendelea kuweka hali ya usafi ndani ya halmashauri hiyo na jiji  la Dar r es Salaam kwa ujumla.
 Amesema watu wamekuwa wakichafua mazingira kwa kutupa taka hovyo hali iliyopelekea mto msimbazi kubeba takataka nyingi zikiwemo ndala,vitatu, chupa, na mifuko ya nail oni,  hivyo amewataka wakazi wa  Wilaya hiyo  kutunza mazingira kwa kuzingatia Usafi.
 "Kama mnavyoona Takataka hizi zote zinatokana na sisi Wana damu mu hivyo wadau wote hawa tuliofika hapa tumejifunza na tunapaswa kutunza mazingira kwa kuweka kwa kutotupa taka ovyo." Amesema Mpogolo.


Amesema kwa wao kufanya Usafi kumewafanya kufikiria kutoa elimu kwa wakazi wa Ilala ili kufahamu namna ya kutunza mazingira kwani wanapofanya usafi wataepusha magonjwa mbalimbali ya milipuko yasababishwayo na Uchafu.
 "Itatusaidia sisi viongozi wa Ilala kupitia kufanya usafi kutatusaidia kutoa elimu namna ya kutunza mazingira na tunapaswa kuchukua hatua kutunza mazingira yetu ya leo kwa manufaa ya halo baadae.
 Aidha amesema wananchi wanapaswa kuwa walinzi wenyewe kwa wenyewe ili kusaidia kutunza mazingira, na kusema kuwa pindi watakapotoa elimu basis wataweka sherWataweka sheria itakayosaidia kulinda na kuhifadhi mazingira.




Kwa upande wake mkuu wa idara ya Mazingira na  udhibiti taka ngumu Manispaa ya Ilala Abron Mapunda amesema eneo hilo Mara nyingi wanalisahau kufanya usafi kwani watu wanatupa taka nyingi katika mto msimbazi na taka hizo zinaenda baharini hivyo amewataka wananchi kuacha kutupa taka katika mto huo.

Naye mwenyekiti wa Mtaa CVU Victor Muneng'i amewashukuru wadau wote waliofika kufanya usafi katika eneo hilo na kuiomba Serikali kuweka mkazo juu ya kutupa taka ovyo pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili kupunguza taka zinazotokana na binadamu.

Katika zoezi hilo limeudhuriwa na wadau  mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa wilaya ambapo imewakilishwa na Katibu tawala, ofisi ya mkurugenzi pamoja na  kampuni za taka na wadau mbalimbali wameshiriki zoezi hilo.

Tazama Picha za wadau mbalimbali wa mazingira walivyokuwa wakijumuika kufanya usafi.

No comments