Ads

WASICHANA 1470 KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI WILAYANI KIGAMBONI


Mwambawahabari 
Na John Luhende 
Mkuu wa  Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa  leo amezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) ikihusisha Wasichana wenye umri wa  kuanzia Miaka 9hadi 14.

Aidha zoezi hilo litaanza rasmi Jumatatu ya April  30 likihususisha zaidi ya wasichana 1470 ambao watakaopata chanjo hiyo katika vituo 113 ikiwemo shule na mitaa, vituo vya afya 23,na vituo 23 vya kutembea maalumu kwa maeneo ya mnada na mikusanyiko 

Amesema utoaji wa chanjo hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukisababisha vifo vya kinamama wengi  huku akiitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara.

Hata  hivyo DC Mgandilwa, ametoa wito kwa viongozi wa Dini, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe kuhamasisha jamii kwenda kupata chanjo hiyo na kuacha tabia ya kudai kuwa ukichanjwa huwezi kupata watoto hizo ni imani potofu 
"Ni wagombea ndugu zangu tushirikiane hili zoezi kwa kuwahamasisha wananchi huko mtaani" alisema

Kwa upande wake Sister Judith Katemba Kaimu Mratibu wa Mama na mtoto Manispaa ya Kigamboni amesema, chanzo cha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuzaa watoto wengi.

 Pamoja na uvutaji wa sigara ambapo dalili zake ni kutokwa na damu bila mpangilio, maumivu ya mgongo, miguu, kiuno, kutokwa na uchafu ukeni pamoja na kuchoka, kupungua uzito na hamu ya kula.


Amesema Saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa na Virusi vya Human Papilloma ambapo kinga yake kwa hatua ya mwanzo ni kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dalili za mwanzo na kupata matibabu stahiki.

Chanjo ya Saratani ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa mwaka 2018 itatolewa kwa wasichana wanaotimiza umri wa miaka 14 ambao wamezaliwa kuanzia January 01 hadi Disemba 31 mwaka 2004.

No comments