Ads

WAKINABABA ZAIDI YA 2,000 WAKUBALI KUTOA FEDHA ZA MATUNZO KWA WATOTO WAO, 90 WAPIMA DNA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM 

Zoezi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda la kuwasikiliza wakinamama waliotelekezwa na wanaume wao limefanikiwa kwa asilimia kubwa baada ya kinababa zaidi 2,000 kukubali kutoa fedha za matunzo kwa ajili ya watoto wao huku 90 wakienda kupima DNA.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini wakati wa kutoa tathimini ya zoezi la kuwasikiliza wakinana waliochiwa watoto na wanaume bila kupewa malezi, Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, amesema kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na mafanikio yaliopatikana.

Amesema kuwa zoezi hilo mpaka sasa limedumu kwa siku 15, huku idadi ya kinamama walioachiwa watoto na wanaume za bila malezi wakiendelea kujitokeza katika ofisi yake tofauti na idadi iliyokuwa inakusudiwa.

Ameeleza kuwa miongoni mwa malengo katika zoezi hilo ni kuwasikiliza wakinamama waliotelekezwa na  wakinababa, wakinababa waliotelekezwa na wakinamama baada ya kuachiwa watoto pamoja na watu waliochana kuachana bila kupata haki zako za msingi.


Katika taarifa yake Mhe. Makonda amesema kuwa zaidi ya familia 17,000 zimejitokeza katika ofisi yake wakiwa na matatizo mbalimbali ambayo yameshindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu, huku idadi ya wakinababa wakiwa 2,000.


 Amesema  kuwa baada ya kusikilizwa kila mmoja wakinababa 2,000 wamekubali kutoa fedha za matunzo kwa watoto wao, huku wengine wamekubali kwenda kupima DNA ili kuthibitishwa ukweli wa watoto wao.


Mhe. Makonda amesema kuwa watato ambao baba zao wameshidwa kupatikana ambao wapo 2,971 watapatiwa bima ya afya bure ili kuhakikisha na wao wanaendelea kupata matunzo.


"Tatizo hilo ni kubwa katika jamii Jambo linalosababisha kuwa na idadi kubwa ya watoto omba omba, wanawake wanaotoa mimba, kuwatupa vichanga, wanaotenda uhalifu wa kuiba, kuwa panya road, kutokana na kukosa matunzo kutoka kwa wazazi wao" amesema Mhe Makonda.


Katika hatua nyengine amesema kuna makundi matatu ya wakina baba walioko katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mengine ambao wakaidi wito watachukuliwa hatua za kisheria ili kuhakikisha wanakamatwa na kuja kuhojiwa.




Hata hivyo Mhe. Makonda ameeleza kuwa kuwa watoto wawili ambao ni wa wachina wameahidiwa kupata huduma za matunzo kutoka kampuni moja iliyopo hapa nchini ambayo inashugulika na ukandarasi ambayo.


Mhe. Makonda amewashukuru wanasheria, waandishi wa habari, na watu wote walioshiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuwataka kuendelea na moyo huo ili kufanikisha maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kuboresha katika ngazi ya familia. 


No comments