Ads

CCM KATA YA UKONGA WASAIDIWA UKARABATI WA OFISI


 Mwambawahabari
Na Mbaraka mwinyi
Chama cha mapinduzi kata ya  ukonga Leo wamepokea msaada wa vifaa na pesa taslim kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya Ccm ya kata hiyo
 Msaada huo umetolewa Leo na katibu wa Elimu na malezi wa jumuia ya  wazazi wilaya ya ilala ndg  Wilson tobola  ikiwa ni ahadi yake ktk kata hiyo aliyoitoa wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya wazazi wilaya ilala ilipofanya ziara ktk kata hiyo hivi karibuni,

Katika makabidhiano ya vifaa hivyo katibu wa Emma alifatana na katibu wa wazazi wilaya ya ilala ndg  Sophia Ahmad  na mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya wazazi wilaya ilala ndg  Abdallah othuman
Vifaa vilivyokabidhiwa ni bati 20,ndoo kubwa za rangi 2,cement mifuko 5,pamoja na misumali kilo 2,vyote vinathamani ya sh 528,400/=

Akizungumza baada ya makabudhiano hayo mwenyekiti wa Ccm kata ya ukonga ndg  mawazo half an alimshukuru katibu wa Emma kwa msaada alioutoa ktk kata hiyo kwani jengo ilo lipo ktk hali mbaya ,alisema ukonga inajivunia kuwa na viongozi wengi wa jumuia hiyo ngazi ya wilaya
"Kipekee nikupongeze katibu wa Emma kwani tangia uingie Katika nafasi hiyo kwa muda mfupi umefanya vitu vingi na ukonga inajivunia sana kuwa na viongozi nyinyi mnaotoka ukonga" alisema mawazo,
Nae ndg tobola alisema kuwa anawashukuru wana ukonga kwa kukubali msaada wake na kusema wao kama jumuia wanafurai kuona wanasaidiana na chama ktk kutatua changamoto zinazoikabili,, "tunawashukuru walezi wetu chama kwa kuwa karibu na sisi na tumeanza kutekeleza ahadi zote tulizoaidi ktk kata wakati wa ziara yetu iliyopita" alisema ndg tobola,
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mazizini kwa niaba ya halmashauri kuu ya kata ya ukonga alimshukuru ndg tobola kwa msaada huo na kumuahidi kuwa nae bega kwa bega ktk ujenzi wa chama na wao kama wenyeviti wa mitaa watachangia sh 150,000 kwa ajili ya fundi,
Katika kuunga mkono juhudi za ukarabati wa jengo ili katibu wa wazazi wilaya ya ilala ndg Sophia Ahmad alichangia sh 100,000 pesa taslim kwa ajili ya ununuzi wa mbao, ambapo ndg tobola aliaidi kununua viti kumi na meza moja wa ajili ya ofisi,

No comments