WASICHANA 24097 KUCHANJWA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI DAR, MAKONDA AZINDUA ZOEZI RASMI.
Mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Mhe. Paul Makonda ametoa wito kwa viongozi wote wa Serikali za mitaa na viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wenye umri wa miaka 14 wafike kwenye vituo kwa wingi kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi unaolengwa kutolewa kwanzia Jumatatu ya wiki ijayo.
Makonda ameyasema hayo leo Aprili 21 wakati akifungua rasmi Warsha ya chanjo hiyo iliyowashirikisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa lengo likiwa kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu na kuweza kusaidia wasichana kujitokeza kwa wingi kupata chanzo hiyo.
Amesema chanjo hiyo itasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na saratani kwani ugonjwa huo umekuwa ukisababisha vifo vingi kwa wanawake.
Chanzo ya saratani ya Mlango wa kizazi inatarajiwa kunza Aprili 23,mwaka huu kwa mkoa huo,ambapo Vituo 270 vitatoachanzo hiyo katika mkoa wa Dar es Salaam, na kulengwa kutolewa kwa wasichana wote wenye umri 14.
Aidha amebainisha kuwa Wakati chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ikitarajiwa kuanza kutolewa Jumatatu wiki ijayo, Rc Makonda amesema ana mikakati ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwapima wanaume saratani ya tezi dume.
Amesema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba ambao hata hivyo hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo katika jamii huku wengine wakiwa na imani za kishirikina kuwa ugonjwa huo ni wa kulogwa.
"Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu kuhakikisha tunapima saratani hii kwa kina baba na kupunguza kasi ya vifo kwa kinababa inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu," Amesema Makonda.
Makonda amesisitiza pia kuzingatia kupata chanjo kamili kwa kurudi mara ya pili ili kuikamilisha kwani wasichana watakaopata chanzo hiyo watatakiwa kupata tena kwa mara nyingine ili kukamilisha kinga
Post a Comment