WAJUMBE WA KAMATI YA UKIMWI MANISPAA YA UBUNGO WAPATA FURSA YA KUPIMA HIV
Upimaji huo umefanyika leo wakati wa ziara ya kamati ya Ukimwi walipotembelea kikundi cha umoja wa wazee Mbezi BAWAZI ili kuona miradi wanayojishughulisha nayo ili kujiongezea kipato.
Kamati hiyo chini ya kaimu Mwenyekiti Diwani mama Mashoto wametembelea miradi miwili ya kikundi hicho ambapo wamejionea mradi wa maji ambao kikundi hicho cha wazee huuza maji hayo kwa wananchi.
Mradi wa pili uliotembelewa ni mradi wa kahawa ambao nao huwaingizia mapato katika kikundi hicho.
Ziara hiyo ni mwaliko wa wazee ambao ni wajumbe wa kamati ya kudhibiti ukimwi katika manispaa ya Ubungo kwa nia ya kutaka waone shughuli wanazofanya.
Akiongea mara baada ya kutembelea miradi hiyo Mwenyekiti Mh. Mama Mashoto amewapongeza wazee hao na kuwataka wasonge mbele bila kukata tamaa.
Akiongea mratibu wa kudhibiti bikini Manispaa ya Ubungo Mercy Ndekeno amewapongeza na kuwataka kutosita kuwasiliana pale wanapopata changamoto ili waweze kusaidiwa.
Katika risala yao wameshukuru kamati kwa kuwatembelea na kuwaomba kuwasaidia katika changamoto ya kukuza mtaji katika uuzaji wa kahawa waweze kufikia hatua ya kuwa na mgahawa kwani ndilo lengo lao.
Kamati pia imepata nafasi ya kupima ukimwi zoezi lililoandaliwa na kikundi hicho cha wazee katika ziara hiyo.
Kamati ya Kudhibiti ukimwi hutembelea vikundi mbalimbali kwa ajili ya kuona shughuli na kusikia changamoto zao ili kusaidia.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO UMC
Post a Comment