CHUO CHA TAIFA UTALII YALETA FURSA SIKU YA TAMASHA APRIL 27 MWAKA HUU.
Watatu kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Shughuli za Kitaalam katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Stephen Madenge akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kimeandaa tamasha la siku ya taaluma lenye ujumbe ‘fursa ya ajira kwa vijana kupitia taaluma ya ukarimu na Utalii’ linalotarajia kufanyika aprili 27 mwaka huu katika Kampasi ya Bustani jijini Dar es Salaam.
Magenge amesema sekta ya utalii nchini haijapungua kwani imeendelea kufanya vizuri kwa kuweza kupata watalii ukilinganisha na nchi zinazozunguka Afrika Mashariki, hivyo wataendelea kutoa elimu ya utalii kwa watanzania.
"Kwa kutumia tamasha hili wanafunzi wataonesha kwa vitendo uhodari wa taaluma zitolewazo chuoni ikiwa ni pamoja na Live Cooking,Cocktail na pastry product makini pamojana na wine testing and testing preparatioin” amesema Madenge.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Eunice Ulomi, amesema kuwa wataendelea kuwafundisha wanafunzi elimu ya utalii ikiwemo utamaduni ili kutangaza asili ya mtanzania jambo litakalosaidia kuwavutia watalii hapa nchini.
“Chuo kinaendelea kutoa mafunzo katika taaluma ya utalii na ukalimu..kufanya hivyo tunaamini kutaendelea kukuza utalii na utamaduni hapa nchini” amesema Ulomi.
Mkuu wa Kampasi ya Temeke Martina Hagweti, amesema kuwa wanaendelea kuwahamasisha watanzania kuwa na dhana ya kujiwekea mazoea ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Chuo cha Taifa cha Utalii ni wakala uliopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo wana dhamana ya kutoa mafunzo ya ukarimu na utalii nchini pamoja kutoa ushauri wa kufanya tafiti.
Post a Comment