NHIF YAJA NA USHIRIKA AFYA ILI KUWASAIDIA WANAUSHIRIKA
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
MFUKO wa Bima ya Afya
nchini (NHIF) umeamua kuanza kutoa huduma za Bima ya Afya kwa wanachama wa Vyama
vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) chini ya Mpango wa Ushirika Afya kwa ajili ya kuwawekea mazingira
ya mazuri ya kuwapatia matibabu mwaka mzima.
Kauli hiyo imetolewa
jana mjini Igunga na Mkurugenzi Mkuu wa NIHF Bernard Konga kwenye mkutano Mkuu
wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Ingembensabo uliofanyika Wilayani Igunga.
Alisema BIMA imeona
kuwa mwanaushirika anakuwa na uhakika wa matibabu kipindi cha mavuno na
anapouza mazao yake lakini baada ya hapo anapata shida na ndio maana wamekuja
na mpango wa kuwasaidia wanachama wa ushirika.
Konga alisema atakayejiunga
na BIMA hiyo atakuwa na uwezo wa kupata matibabu katika vituo 6995 ambavyo
Mfuko huo umeingia navyo mkataba nchini kote kwa ajili ya kuwahudumia wanachama
wake.
Aliongeza kuwa
mkulima uwa na msimu mmoja katika mwaka mmoja na unapokwisha ungojea mwaka
mwingine ndio apate fedha jambo ambalo linawafanya wauze mali zao kama vile
mashamba ili kupatiwa matibabu.
Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza
kuwa kwa kuanzia Mfuko huo utaanza na Ushirika ulio katika mazao makuu matano
ya biashara ambayo ni pamba, tumbaku, chai kahawa na korosho na baada ya hapo
watakwenda ushirika mazao mengine.
Konga alisisitiza baada ya mazao hayo watakwenda kwenye
wanaushirika wengine kwa lengo ni
kuwafikia Wanaushurika wote ili waweze kufanyakazi zao za uzalishaji wakiwa na
afya bora na kuwa na uhakika wa matibabu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Aggrey Mwanri alitoa kwa mifuko mingine ya bima kuangalia hata wa
uwezekano wa kuzikatia Bima majumba ya kuhifadhia mazao ya wakulima ili
kuwakinga na hasara pindi yakitokea majanga kama vile moto.
Post a Comment