ILALA YA WATAKIWA KUONGEZA KASI URASIMISHAJI ARDHI
Mwamba wa habari
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Kate Kamba ameitaka idara ya ardhi wilaya ya Ilala kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa juhudi zaidi ili kuondoa tatizo la kutorasimishwa kwa maeneo mbalimbali hapa nchini hasa miji inayokua ambayo baadae ianakuwa kero kwa wananchi.
Aidha katika ziara hiyo iliyowahusisha madiwani, viongozi wa CCM Ilala pamoja na wakuu wa idara imetembelea miradi ya ujenzi wa shule za juhudi na uhuru mchanganyiko na kisima cha maji cha kisukuru ambapo amewataka madiwani kushirikia kikamulifu kwenye ujenzi wa miradi hiyo ili kugundua mapungufu na kuyafanyia marekebisho kwa haraka.
Mwenyekiti CCM mkoa Bi. Kamba ameitaka halmashauri kuangalia jinsi ya kupunguza gharama za ujenzi wa miradi na iwe katika hali ya ubora ikiwemo kuondoa gharama zisizo za lazima kwa kutumia mafundi wa maeneo husika kwa bei nafuu pamoja na kununua saruji zisizotozwa kodi.
Sambamba na hayo bi Kamba ameutaka pia uongozi wa wilaya ya Ilala kuangalia njia nzuri za kuwasaidia vijana wanaoendesha bodaboda kufanya kazi zao kwa ufanisi bila kuvunja sheria kwani wanategemewa kwenye utunzaji wa familia pamoja na ukamataji unauzingatia utaratibu maalumu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia mjema amesisitiza kuwa wilaya ipo salama na kuwakaribisha wawekezaji kuja kwa wingi na kuahidi kushirikiana nao kwa karibu zaidi ili kukuza uchumi wa nchi na pale itakapogundulika uvunjifu wa amani taarifa zitolewe ili wahusika wachukuliwe hatua.
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amemshukuru mwenyekiti wa mkoa kukubalia kutembekea miradi hiyo na kumdhibitishia kuwa mahusiano yao na halmashauri yapo vizuri na mapungufu yaliyojitokeza yatarekebishwa.
Hata hivyo ameongeza kuwa kutokufikia malengo yaliyokusudiwa ni kutokana na upatikanaji mdogo wa fedha kutoka serekalini pamoja na kutofika kwa wakati hivyo kuomba usimamizi mzuri wa bajeti ili kupatikane fedha za kutosha.
Post a Comment