EPZA , TCCIA KUSHIRIKIANA KUHAMASISHA UWEKEZAJI
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji
wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA), James
Maziku akielezea majukumu ya mamlaka hiyo mbele ya wajumbe wa Taasisi
ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA) walipofanya ziara katika
mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ililenga kuwajengea
uwelewa wa pamoja ili kuhamasisha wazawa zaidi kuwekeza katika maeneo
hayo.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum
wa Uwekezaji(EPZA), Nyanda Shuli akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa
Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) walipofanya
ziara katika mamlaka hiyo jana jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo ililenga
kuwajengea uwelewa wa pamoja ili kuhamasisha wazawa zaidi kuwekeza katika
maeneo hayo.Kushoto ni Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA Bi.
Grace Lemunge.
Baadhi ya wajumbe kutoka Taasisi ya Biashara,
Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu
fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia Mamlaka ya Ukanda Maalum wa
Uwekezaji(EPZA) wakati wa ziara katika mamlaka hiyo jana jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Biashara, Viwanda na
Kilimo Tanzania, wilaya ya Ubungo Bw. Clement Bocco akimsikiliza Meneja
Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd, Rigobert Massawe,
walipotembelea kiwanda hichi ikiwa ni ziara yao ya kutembelea Mamlaka
ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA) Benjamin Mkapa EPZ Ubungo External
jijini Dar es Salaam jana. Kiwanda hicho kinatengeneza nguo aina ya
Jeans na kuziuza katika masoko ya nje.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Tanzania
Tooku Garments Co. Ltd wakiendelea na shughuli za ushonaji wa nguo ambaozo
baadaye usafirishwa nje ya nchi. Kiwanda hicho kipo katika eneo la uwekezaji
la Benjamin Mkapa EPZ, Ubungo External jijini Dar es Salaam yalipo Makao
Makuu ya Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji(EPZA).
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa
za mazao ya nafaka Somani Agro Export Ltd (SAEL), Dkt. Alykhan Somani
akielezea jinsi mazao hayo yanavyochakatwa katika madaraja tofauti tayari
kwa kuuzwa nje ya nchi alipotembelewa na wajumbe wa Taasisi ya Biashara,
Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) jana jijin Dar es Salaam. Wajumbe
hao wa TCCIA walifanya ziara katika ofisi za Mamlaka ya Ukanda Maalum
wa Uwekezaji(EPZA) kwa lengo la kujengewa uelewa na kuangalia namna
wanavyoweza kushirikiana.
Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Mamlaka ya Ukanda
Maalum wa Uwekezaji(EPZA) Bi. Grace Lemunge (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa Taasisi ya Biashara, Viwanda
na Kilimo Tanzania (TCCIA) mara baada ya kumaliza ziara yao katika Ofisi
za mamlaka hiyo jana jijini Dar es Saalam.(Picha zote na: Frank Shija
- MAELEZO)
Post a Comment