Ads

KAMPUNI YA MBOLEA YARA TANZANIA LTD YATOA PUNGUZO ASILIMIA 50 KUWASAIDIA WAKULIMA.

02
01
Meneja Masoko wa Kampuni ya Usambazaji wa Mbolea ya Yara Tanzania Ltd nchini Linda Byaba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

MWAMBA WA HABARI
HUSSEIN NDUBIKILE NA ISAAC MAGESA, DAR ES SALAAM.
KAMPUNI ya Usambazaji wa Mbolea ya Yara Tanzania Ltd imetangaza punguzo la bei ya mbolea ya YaraMila Otesha kwa asilimia 50 huku ikibainisha lengo lake ni kuwawezesha wakulima kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni hiyo nchini Linda Byaba, amesema punguzo hilo litawasaidia wakulima kumudu gharama za mbolea itakayowazesha kupata mavuno mengi ukilinganisha na mbolea nyingine ambazo hazina ubora unaotakiwa.

“ Mbolea hii tuliizindua mwaka jana ina virutubisho saba ,sifa ya kuyeyuka  haraka kwenye udongo, uwezo wa kufanya kazi ndani ya siku mbili hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja kutochachusha udongo,” amesema.

Byaba amesema mbolea hiyo ina ubora wa kupandia mazao ya aina zote ikiwemo Mahindi, Chai,Sukari, Alizeti,Tumbaku, Mpunga, Viaz na Mbogambogai huku akibainisha asilimia 50 ya wakulima waliokwishaitumia imewaongezea uzalishaji wa mazao.

Amebainisha kuwa mbolea ya YaraMila Otesha ina virurubisho saba na kwamba kila punje moja ya mbolea hiyo ina virutubisho vyote vikiwemo Nitrojeni, Fosiforasi, Kalsim , Boroni na Magneziam.

Amefafanua kuwa mbolea hiyo inapatikana dunia nzima huku akitilia mkazo wakaulima wa mbogamboga na nafaka katika nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi wanafafaidika nayo.

Aidha, amesema sifa nyingine za mbolea hiyo ni kuchochea machipukizi mengi yanayoleta mavuno mengi katika zao la mpunga, utoaji mizizi mingi, hivyo kuufanya mmea kuwa imara muda wote pamoja na kuwa na kiwango cha juu kirutubisho cha Fosforasi ukilinganisha na mbolea nyingine za kupandia.

Ameawashauri wakulima kuachana na mbolea zilizopitwa na wakati na zizizo na virutubisho sahihi kwani mbolea ya kampuni hiyo hutoa majibu haraka.

Ameeleza kuwa mbolea hiyo husambazwa kupitia usafiri wa reli, mawakala wakubwa wa mbolea kwa kutumia usafirishaji  wa malori.

No comments