MITAMBO YA UMEME YAFANYIWA MAREKEBISHO
MWAMBA WA HABARI
Na mwandishi wetu
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema hali ya umeme kwa sasa ni wastani na hakuna mgao.
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani
Amesema hayo katika kipindi cha tunatekeleza na kusema “ Si kwamba tuna mgao wa umeme, tunarekebisha mitambo ya umeme iliyodumu kwa takribani miaka 40.”
Amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwapo na mitambo ya umeme itakayowezesha kutoa huduma ya umeme kwa uhakika na kuwa umeme ni uchumi na huwezi kutenganisha masuala ya maendeleo na nishati.
Waziri hiyo amesema upungufu wa umeme unatokana na ukarabati unaoendelea na mafundi hawalali kuhakikisha hali inakuwa sawa.
“Hadi kufikia Desemba 15,2017 tutakuwa tumefanya ukarabati katika sehemu kubwa na kutakuwa na tofauti kubwa,’’ amesema
Pia amesema hadi kufikia mwezi wa 1 au wa 2, 2018 mkandarasi wa kujenga stiegler's gorge atapatikana na kuanza ujenzi. Mradi wa stiegler's gorge utazalisha megawati 2100 kwa mkupuo.
Amesema mradi wa Kinyerezi 2 umekamilika kwa 86% na kuanzia mwezi huu utaanza kutoa megawati 30 kila mwezi.
Mradi wa umeme Makambako-Songea ni mradi mkubwa utakuwa na vituo 3 vya kupoozea umeme, utakamilika Septemba mwakani.
Waziri huyo amesema katika REA 3 serikali itahakikisha kila kijiji kinapata umeme na kwamba vijiji zaidi ya 7,000 havijapata umeme
"Mpaka kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vitakuwa vimepata umeme,’’ amesema

Post a Comment