Ads

NEC yaanza maandalizi uboreshaji wa daftari la wapiga kura

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye kituo cha redio Dodoma FM cha mjini Dodoma.Kulia kwake ni Afisa wa Tume Bw. Mawazo Bikenye na mbeye ni watangazaji .Picha na Hussein Makame, NEC-Dodoma.

Hussein Makame-NEC, Dodoma 
Mwambawahabari
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 baada ya Serikali kutenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kazi hiyo katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani kwa nyakati tofauti wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika vituo vya redio vilivyoko mkoani Dodoma.
Alisema kuwa maandalizi ya uboreshaji huo ni pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio nchi nzima mpango ambao umeanza kutekelezwa kwa baadhi ya mikoa nchini. 
 Tume imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Serikali imeshatenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2017/2018alisema Bw. Kailima.
Aliongeza kuwa kwa kipindi hicho Tume itatoa kadi mpya ya mpiga kura kwa watakaoandikishwa upya, waliopoteza kadi na kadi zilizoharribika, kwa wanaohamisha taarifa zao ikiwemo waliohamia Dodoma, na kufuta wapiga kura waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura.
Bw. Kailima aliwataka wananchi wafuatilie elimu ya mpiga kura inayotolewa kupitia redio ya mikoani kuelewa mambo mbalimbali yanayohusu mchakato wa uchaguzi ili fikapo mwaka 2020 kila mwananchi awe ameelimika na asiweze kupotoshwa.
Alisema kwamba kwa muda mrefu elimu ya mpiga kura imekuwa haitolewa kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.
Alifafanua kuwa Ibara 74 (6) (e) ya Katiba inaitaka Tume kutekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria nyingine yiyite iliyotungwa na Bunge na Ibara ya 18 inampa kila mwananchi haki ya kupata taarifa muhimu zinazohusu nchi yake

No comments