WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA JUMLA YA MILIIONI 12 MCHANGO KWA SERENGETI BOYS KUTOKA MULTICHOICE TANZANIA, MISA TANZANIA NA TAKUKURU
Mwambawahabari
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kupokea mchango kwa ajili ya
Timu ya Mpira wa Miguu ya Serengeti Boys kutoka kwa wadau wa michezo
nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea hundi ya Shillingi
Millioni 10 leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Kampuni ya Multichoice
Tanzania iliyowasilishwa kwa niaba yao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo Dkt.Hassan Abbas.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea mchango wa Shillingi
Millioni moja kwa ajili ya Serengeti Boys leo Jijini Dar es Salaam
kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
Tawi la Tanzania Bi. Salome Kitomari.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea mchango wa Shillingi
Millioni Moja kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini
(TAKUKURU) iliyowasilishwa kwa niaba yao na Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.
Picha na Shamimu Nyaki WHUSM.
…………………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea jumla ya
shilingi 12,000,000 kutoka kwa Kampuni ya Multi Choice,
Taasisi ya Vyombo vya Habari
Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) pamoja na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kuisaidia timu ya
Serengeti Boys.
Dkt. Mwakyembe amezipokea fedha
hizo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kuahidi
kutoa taarifa ya kiasi cha fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali
mwishoni mwa mwezi huu.
“Nawashukuru wadau wote
wanaoendelea kuichangia timu yetu ya Serengeti Boys, leo nimepokea
shilingi 10,000,000 kutoka Kampuni ya Mult Choice, shilingi 1,000,000
kutoka MISA TAN pamoja na shilingi 1,000,000 kutoka TAKUKURU”, alisema
Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa timu imeanza
mashindano hayo vizuri japokuwa wametoka bila kufungana na timu ya Taifa
ya Mali ambayo ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.
Aidha, ameahidi kuwa mchezo dhidi
ya Timu ya Serengeti Boys na Timu ya Angola itakayochezwa Mei 18 mwaka
huu itarushwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
MISA TAN, Salome Kitomari amesema kuwa waandishi wa habari wameamua
kuisaidia timu hiyo sio kwa kutumia kalamu zao kuwatangaza katika vyombo
vya habari tu bali imeamua kuwasaidia kwa kuwachangia fedha.
“Tumeamua kuichangia timu yetu
ili tuwape moyo zaidi wa kufanya vizuri kwani wameonesha jitihada katika
mchezo wa mpira wa miguu,” alisema Bi. Salome.
Post a Comment