Ads

TAMASHA LA BODA BODA SUPERSTAR LA FANA DAR.

Mwambawahabari

picha ya Dereva boda boda akishiriki shindano LA kuvuka vizuizi

Baadhi ya Wananchi  walijitokeza kushudia mashindano hayo.

Mkurugenzi mkaazi wa IRI Tanzania akizungumza na  waandishi wa habari.

Meneja mkuu wa kampuni ya JP Decaux aliyevaa suti kushoto akisakata rumba baada ya muziki wa singeli kumkosha

Bodaboda iliyoshindaniwa na kuchukuliwa na mmoja wa madereva boda boda aliyefahamika kama baba Aisha wa kawe

Msanii wa muziki wa singeli Shoro Mwamba na kundi lake
Mwambawahabari

Maelfu  ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viunga vyake pamoja na wakali wa boda boda  Jana wamejitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho kubwa LA madereva wa boda boda katika viwanja vya Tanganyika packes (Kawe) lililoandaliwa na kampuni ya JP Decaux kwa ushkrikiano na shirika la IRI na kudhaminiwa na Pepsi,NMB,Sayona,StarTimes,Meku one,Nyemo Fm na Sibuka Fm.

Awali katika tamasha hilo meneja Mkuu wa kampuni ya JP decaux,SHABAN MAKUGAYA amewaambia wanahabari kuwa lengo la tamasha hilo ni kumtafuta dereva bora wa boda boda katika mkoa wa Dar sambamba na kutoa elimu kwa madereva hao kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ili kuwasaidia madereva
hao katika ufanyaji wa kazi zao na kuepuka ajali zinazotokana na ukosefu wa elimu ya usalama barabarani ambapo ambapo madereva wengi walijitokeza kushiriki

Naye mkurugenzi mkaazi wa taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masula ya amani (IRI) Bi ROBINA NAMUSISI amesema tamasha hilo pia limetengeneza mahusiano mazuri kwa kuwakutanisha watu wa matabaka mbali mbali pamoja na kuendeleza amani ya Taifa hivyo taasisi yake itaendelea kushirikiana na JP decaux katika matamasha hayo ambayo yatafanyika nchi nzima.

Aidha kwa upande wake diwani wa kata ya kawe,MUTA RWAKATARE amewaambia wanahabari kuwa wakazi wa kata yake wamelipokea tamasha hilo kwa mikono miwili kwani mbali na kutoa elimu kwa madereva boda boda pia limesaidia kuwaunganisha madereva hao sambamba na kusaidia kupunguza matukio ya uhalifu kutokana na madereva hao kujuana na kufanya kazi pamoja kwa amani.


Meneja mkuu wa JP Decaux SHABAN MAKUGAYA (Kushoto)akiwa na mkurugenzi wa michezo kutoka wizara ya habari Sanaa utamaduni na Michaezo,YUSUPH SINGO OMARY aliyekaa katikati na diwani wa kata ya kawe MUTA RWAKATARE aliyekaa kulia


Tamasha hilo ambalo limefanyika kwa Mara ya kwanza jijini Dar pia lilitanguliwa na mechi ya kirafiki kati ya madereva boda boda na askari wa kikosi cha  usalama barabarani (Trafiki)ambapo matokeo yaliwapa ushindi Trafiki baada ya kuwatandika madereva hao mabao 2 huku madereva hao wakiambulia goli 1 la kufuata machozi sambamba na kumzawadia piki piki ya King Lion Dereva boda boda aliyeshinda katika kujibu maswali ya masuaka ya usalama barabarani vyema.

No comments