DIAMOND PLATNUM KUTUMBUZA UFUNGUZI WA MASHINDANO YA AFCON NCHIN GABON
Na Maria Kaira,
Mwambawahabari
Wizara ya Habari Utamaduni , Sanaa na Michezo , imefanikisha safari ya Mwanamuziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nasibu Abdul (Diamond) katika kufanikisha onyesho lake katika ufunguzi wa mashindano ya AFCON nchini Gabon.
Michuano hiyo imedhaminiwa na kampuni ya Total inayotalajiwa kuanza January 14 na fainali itakuwa Februari 5
Mwaka huu.
Mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Salum Salum amesema Diamond ni miongoni mwa wasanii teule watakaotumbuiza katika hafla hiyo kitendo ambacho kimechukuliwa na watanzania wengi kuwa ni fursa ya Tanzania kusikika katika mashindano hayo japokuwa timu yetu haikuweza kufuzu kushiriki.
Pia amesema mtifuano huo wa AFCON mwaka huu unafanyika katika nchi ndogo ya Gabon, huku jumla ya timu 16 zikishiriki ikiwemo Uganda ambayo ndiyo timu pekee iliyofuzu kutoka Afrika Mashariki.
Michuano hiyo inanogeshwa zaidi na uwepo wa wachezaji nguli ulimwenguni hususan wale wanaochezea vilabu vikubwa kama Manchester United, Arsenal, Chelsea, Real Madrid na vilabu vingine vikubwa duniani. Wababe wa kabumbu kama Mohamed Elneny, Eric Bailly, John Obi Mikel, Pierre Aubemayang, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Victor Moses ni miongoni mwa vigogo watakaoonyesha umahiri wao katika michuano hiyo.
Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Mh. Nape Nnauye amesema kuwa, kuwepo kwa Diamond kwenye uzinduzi wa michuano hiyo ni kitendo cha kujivunia na kwamba Serikali ikishirikiana na DStv imefanya jitihada kubwa kufanikisha safari ya WCB kuelekea Gabon.
Kwa upande wake Diamond ameishukuru Serikali na DStv kwa ushirikiano wao hususan kufanikisha safari yao ya kuelekea Gabon. Aliongeza kuwa jitihada binafsi za Waziri wa Habari ziliwezesha zoezi hilo kufanikiwa na kwamba wanaahidi kuwa hawaendi kama WCB, bali kama watanzania na watahakikisha kuwa wanaipeperusha vema bendera ya Tanzania katika onyesho hilo.
Post a Comment