TEA Yatoa Milioni 496 Kujenga Uzio wa Hosteli Mpya za UDSM.
Na Lilian Lundo
mwambawahari
Mamlaka ya Elimu Tanzania Tanzania (TEA) imetiliana saini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkataba wa ujenzi wa uzio katika hosteli za Mwalimu J.K. Nyerere Kampasi ya Mlimani.
Mradi huo umedhaminiwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu (Education Fund) utakaogharimu jumla ya shilingi 496,646,868 hadi kukamika kwa ujenzi huo.
Mkataba huo umesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDSM Profesa Rwekaza Mukandala wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa utekelezaji mradi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Kwa upande wake Prof. Mukandala aliwashukuru TEA kwa msaada huo na kuongeza kuwa ujenzi wa uzio hizo ni suluhisho kubwa kwa wanafunzi watakaoishi katika eneo la kampasi hiyo.
Alisema kuwa uzio utasaidia kuimarisha usalama wa wanachuo na mali zao kutokana na kuwepo eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu unaotokana na stendi ya mabasi ya simu 2000 , maduka ya Mlimani City pamoja na viwanja hivyo kutumika kama njia ya mkato na vijiwe kwa watu wasio na kazi.
TEA tayari imefadhili miradi mbalimbali Chuo Kikuu cha UDSM ikiwemio ujenzi wa vyumba vya mihadhara, ununuzu wa vitabu vya kiada, vifaa kwa ajili ya wanafunzi kwenye mahitaji maalum, ufadhili wa kozi za "Pre Entry" kwa wanafunzi wa like katika masomo ya sayansi, ununuzi wa mitambo na vifaa vya Tehama.
Post a Comment