Ads

UTAFITI KATI YA WANAWAKE 100 WANAOISHI MIJINI 42 WANA UNENE ULIO PITILIZA.




Na Maria Kaira,Dar 
mwambawahabari
Imeelezwa kuwa kati ya wanawake 100 wanaoishi mijini inasadikika kuwa  42 wamekuwa na uzito uliopindukia kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Hayo yamebainika leo katika Uzinduzi wa matokeo ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria kwa mwaka 2015/2016.

Akizungumza Mara baada ya kutokea matokeo ya utafiti huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema umefika wakati sasa kuhakikisha wanawake mijini wanajikinga kwa kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza yatokanayo na unene uliopindukia.

"Wanawake wa mijini hii ni kengele ya hatari, wanawake wa vijijini ni asilimia 21 pekee kwenye uzito uliozidi, mazoezi ni muhimu Desemba 21 tutazindua kampeni ya kufanya mazoezi, Wizara ya Afya tumejipanga sasa tunaanza kudhughulika na kinga, shine wanawake tufanye mazoezi kupunguza uzito wa miili yetu kuepuka maradhi," alisema Mwalimu.

Asha Salum ni mmoja wa mwananchi amesema anatoa wito kwa wanawake kujikita katika kufanya mazoezi ili kuweza kupunguza uzito na kuachana na tabia ya kujibweteka.

No comments