Makonda auagiza Uongozi Kariakoo kusikiliza kero za wafanyabiashara
Na John Luhende
mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ameuagiza Uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuitisha mkutano wa wanahisa haraka ili kusikiliza kero na malalamiko ya wafanyabiashara wa soko hilo.
Makonda ameyasema hayo alitembelea Soko la Kariakoo na kusikiliza kero za wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko hilo lililopo wilayani Ilala.
katika ziara hyo, wafanyabiashara hao wamemweleza kuwa wamekuwa wakitozwa ushuru mkubwa kwa siku wa kati ya shilingi 7500 hadi wengine 10,000 huku kila mfanyabiiashara akitozwa shilingi 15,000 kwa ajili ya kitambulisho.
Wamemwomba Mkuu wa Mkoa kutazama upya mpango huo ili nao waweze kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yao kupitia biashara wanazofanya ili kujipatia kipato na kuchangia pato la taifa.
Akizungumza na wafanyabaishara hao katika Mtaa wa Congo jijini humo, Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wafanyabiashara hao kuchagua uongozi wa mpito na kuweka mikakati ya kuwa na umoja wenye nguvu.
Aidha, amewahimiza kuanzisha viwanda vidogovidogo vitakavyozalisha bidhaa na kuviuza hapa nchini badala ya kuendelea kununua bidhaa toka nje ya nchi na kwamba katika kufanikisha hilo yeye mwenyewe ameahidi kuchangia shilingi milioni 100.
Katika hatua nyingine, Makonda amewataka wafanyabiashara wa kigeni kufanya biashara kubwa na ndogo kuwaachia wazawa badala ya sasa ambapo baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni wamejiingiza katika biashara ya umachinga.
Post a Comment