TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAFANYA USAILI KUWAPATA MRATIBU NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI, ZANZIBAR LEO
Mwambawahabari
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan
(katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume wakati
wa kikao cha Usaili wa nafasi ya Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la
Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjata.
Baadhi
ya Wajumbe wa Seckretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakifuatilia kwa
makini zoezi la Usaili wa kuwapata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipitia vyeti na nyaraka mbalimbali wakiongozwa
na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati
wa Usaili wa nafasi ya Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la
Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.
Wajumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakiendelea na zoezi la Usaili kwa waombaji wa nafasi Mraratibu na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la
Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.
Mmoja
wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Mratibu wa Mkoa katika Uchaguzi mdogo
wa Jimbo la Dimani Bw. Salum Juma Mgunya akijieleza wakati wa Usaili mbele ya
Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini
Zanzibar.
Mmoja
wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Msimamizi wa Uchaguzi katika
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bi. Fatma Gharib Haji akijieleza wakati wa
Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi
leo mjini
Wajumbe
wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia zoezi la Usaili la kumpata Mratibu na Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Dimani Zanzibar. PICHA/ Aron Msigwa – NEC.
Post a Comment