SHINDANO LA USHAIRI LA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZA DESEMBA 19
Washairi wa kiswahili wa jiji la Dar es salaam wametakiwa kushiriki katika shindano la pili la tunzo ya ushairi ya mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam linalotalajia kuanza Desemba 19 na kufungwa Desemba 20 ikiwa na lengo la kuienzi historia ya jiji la Dar es salaam na mchango wa meya wa kwanza mwafrika sh. Kaluta Amri Abedi ambaye alikuwa mshairi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jiji hapa Mwenyekiti wa tunzo za ushairi wa mstahiki meya wa Jiji la Dar es salaam Chata Michael amesema kupitia shindano hilo litachangia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha maendeleo ya Jiji la Dar es salaam , pia itachangia kufufua sanaa ya ushairi katika jiji hilo ili iweze kutumika kama burudani na kutoa elimu na maendeleo ya wakazi wote wa jiji la Dar es salaam.
Pia amesema shindano hilo litawahusisha washairi kutoka jiji la Dar es Salaam, na mada kuu itakayohusika katika shindano hilo ni "Jiji La Dar es salaam"kuhusiana na Changamoto na raha za jiji hilo na kila shairi linatakiwa lizingatie mada ndogo tofaititofauti.
"Tunataka shairi liwe la mtunzi mwenyewe asichukue la mtu mwingine, shairi liheshimu miiko ya kijamii na kimaadili na kila mshairi awasilishe mashairi mawili" amesema
Aidha Michael ameongeza kuwa shindano hilo litakuwa la utunzi wa ushairi katika lugha ya kiswahili pekeyake, pia mshairi shariti awe mkazi wa Mkoa wa Dar es salaam.
" tungo zitakazo shindanishwa ni aina ya mashairi ya kimapokeo tu tenzi na nyimbo hazitahusika" amesema
Post a Comment