Ads

MAKONDA AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM KUJITOKEZA KWA WINGI KATI KA SHEREHE ZA UHURU 9 DISEMBA.


rc-makonda-uhuru-4

mwambawahabari

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru yatakayofanyika Desemba 9 Mwaka huu katika Viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuunga Mkono viongozi waliotangulia na waliopo kwa kuilinda na kuitunza amani ya nchi.

Mheshimiwa Makonda ameeleza kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika tangu serikali ya awamu tano iingie madarakani, maadhimisho yatapambwa na kauli mbiu ya Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Kuimarisha Uchumi ambapo mheshimiwa   Makonda amewataka watanzania kuibeba kauli mbiu hiyo na kupambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo ili taifa liweze kusonga mbele na kuifikia hadhima ya Rais Magufuli kwenye Tanzania ya Viwanda ambayo itapatikana bila kuwepo kwa rushwa na ufisadi.

RC Makonda ameongeza kuwa Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo anataraji kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, ambaye atashuhudia shughuli mbalimbali katika viwanja hivyo na kulihutubia Taifa.

No comments