Ads

WASLAM WATAKIWA KUSHEREHEKEA SIKUKUU KWA KUDUMISHA AMANI


Image result for picha za sheikh alhad

Na John Luhende 
mwambawahabari
Rais mstaafu wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania  Alhaji Ali Hassani  Mwinyi  anatarajiwa kuwaongoza waislamu katika siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa dini ya kiislaam mtume muhamad s.w alaih wasaal ifikapo  disemba  11 maulidi ambayo  kimkoa yatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dare s salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari   jijini dar es salaam sheikh mkuu wa mkoa wa dar es  salaam ALHAD MUSSA SALUM amewaka waumini wa dini ya kiislamu kusherehekea mauli hayo kwa njia ya amani na usalama kama ilivyo amrishwa ya mtume muhamadi  kwa waumini wake.



 Amesema maulid hayo yataambatana na maandamano ya amani ambayo yatahamasisha suala la amani nchini yakifuatana na kauli mbiu isemayo muisalamu badilika amani na utulivu ndio maisha yetu.


Maulid ya kuzaliwa kwa mtume  muhamadi kitaifa yatafanyika katika mkoa wa singida hivyo ametoa wito kwa waumini wote wa kiisalamu nchini kuungana na waislamu wote duniani  kusherehekea na kuonesha heshima ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo.

No comments