WAZIRI UMMY MWALIMU KUWA MGENI RASMI HEALTH SUMMIT
Na Rayusa Yasini.
Mwambawahabari
WAZIRI wa Afya jamii ,jinsia, wazee na watoto anatarajiwa kufungua kongamano la Tatu la Kitaifa la afya lijulikanalo kwa
jina la Tanzania Hearth Summit.
Akizungumza Leo jijini
Dar es Salaam Rais wa kongamano hilo Dr Omar Chino amesema mada mbalimbali
zitazungumzwa kutoka kwa washiriki 142 ambao mpaka sasa wamethibitisha ushiriki
wao.
Chino amesema sheria
za usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi katika Tanzania na hali
ilivyo kwa sasa pamoja na nini kifanyike ili kuboresha hali ya afya.
Kuelekea kwenye huduma
ya afya kwa wote, mchango wa taasisi za uma na binafsi zitaongelewa ili kuona
jinsi tutakavoendelea.
"Mpango wa kuelekea
kuwa kituo cha ubora katika magonjwa ya moyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
".
Ameongeza kuwa
jitihada za Tanzania za kufikisha malengo ya maendeleo ya kimkakati ya maisha
yenye afya njema yatazungumzwa kwa pamoja na kupata muafaka.
Kongamano la afya
litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere utakaozihusisha taasisi za MoH
,TMHS, na Baraza la kiislam Tanzania BAKWATA.huku wadau wa afya wakiombwa
kuendelea na usajili kupitia WWW.ths.or.tz.
Mkutano huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya, zinatarajia pia kushiriki katika maonesho ya bidhaa zinafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.
Post a Comment