Ads

KITUO CHA TIBA YA MAGONJWA YA MOYO CHA JAKAYA KIKWETE MUHIMBILI KUTUMIA BURE HUDUMA YA INTERNET KUTOKA TTCL.


Na Angelina Faustine
Mwambawahabari
KAMPUNI ya simu ya TTCL imezindua huduma ya  wi-fi bure katika kituo cha moyo cha Jakaya Kikwete  kilichipo hospital ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii na kupata taarifa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Waziri Kindamba alisema kuwa huduma hiyo itasambaa pia katika bustani,vituo vya mabasi na kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi

“TCCL ina jukumu kubwa la kupeleka taarifa na tunajipanga katika kuboresha huduma za wi-fi katika mkoa wa Dar es salaam na badae tutahakikisha tumefika nchi nzima ili watanzania wengi wapate taarifa na kujua dunia inaendaje”. Alisema Kindamba.


Aliongeza kuwa hakuna haja ya wakazi wa dar es salaam kusongamana sehemu moja au kutoka eneo moja kwenda nyingine kwa ajili ya kufata huduma ya wi-fi ya bure badala yake kampuni hiyo itahakikisha inaibuka kidedea katika ushindani kwa kupitia mtandao.

Aidhaa alisema kuwa nchi ya Tanzania itakuwa nchi ya pili kwa Afrika Mashariki na ni nchi ya tano kwa Afrika nzima ambapo Rwanda na  Afrika ya kusini ni baadhi ya nchi ambanzo wananchi wake wanapata huduma ya wi-fi ya bure kwa baadhi ya maeneo

Alisema kuwa mawasiliano ndio kila kitu katika biashara kwani watu wengi wamekuwa wakitumia mawasiliano katika mitandao mbalimbali ya kijamii kununua na kuuza bidhaa, hivyo ni jukumu lao kama wadau wa mawasiliano kuhakikisha wanawapa watanzania kile wanachokipenda.

No comments