Ads

TANGAZO MUHIMU

MATEMBEZI YA HISANI KUHAMASISHA UCHUNGUZI NA KUCHANGIA TIBA YA SARATANI YA MATITI 29 OKTOBA 2016

Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana na Hoteli ya Kunduchi Beach na Hospitali ya Agha Khan na Radio ya Efm imeandaa matembezi ya hisani tarehe 29 Oktoba, 2016 ambayo yataanzia katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road saa 12.30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4.30 katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Mgeni Rasmi atakuwa Mheshimiwa Dkt. Hamis Kingwangalla (MB), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Lengo la matembezi hayo ni kuongeza uelewa kwa jamii juu ya saratani ya matiti na kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba ya dawa za dripu (chemotherapy) na hivyo kuchangia juhudi za Serikali katika kuimarisha tiba ya saratani ya matiti nchini.
Pia huduma ya uchunguzi wa saratani ya matiti itatolewa bure na uchangiaji damu kwa ajili ya wagonjwa wa saratani.


Kuchangia kwa M- Pesa Namba 175555, Fuata Maelekezo

 Piga *150*00#  (b) Chagua 4, Lipa kwa M-Pesa (c) Chagua 4, Namba
 ya Biashara, (d)  Ingiza Namba ya Kampuni 175555
(e)  Ingiza Namba ya Kumbukumbu 175555 (f) Ingiza Kiasi cha Fedha
(g) Ingiza Namba ya Siri (h) OK

Kuchangia kwa Tigo – Pesa, Tuma Namba 0719 80 33 44

Weka Mchango wako katika Akaunti ya Taasisi:

Jina: Ocean Road Cancer Institute,
Jina la Benki: KCB Bank Tanzania Ltd,
Namba ya Akaunti:  3301248489,
Tawi: Samora

Wote mnakaribishwa kushiriki.
OKOA MAISHA WAHI HOSPITALI UKAFANYIWE UCHUNGUZI MAPEMA

Imetolewa na
MKURUGENZI MTENDAJI

No comments