Ads

MSEMAJI WA SERIKALI: MUSWADA WA HABARI UTATOA FURSA KWA CHOMBO CHA HABARI KUOMBA RADHI PASIPO KUCHULIWA HATUA NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA



Mwambawahabari
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
SERIKALI imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.

“Sifa moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea  hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.


Aidha Abbas alisema kuwa ipo misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

Aidha Abbas aliongeza kuwa muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa wanahabari kwani unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa habari ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari pekee.


Mkurugenzi Abbas alisema kila taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati kwa Tanzania napo kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki taaluma  ya habari.

No comments