SERIKALI YAIPONGEZA QUALITY GROUP KWA KUANZISHA KITUO CHA URITHI WA UTAMADUNI TANZANIA (TCCH)
mwambawahabariblog
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Qaulity Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Na: Frank Shija;WHUSM
Serikali yaipongeza
Kampuni ya Quality Group ltd kwa hatua yake ya kuanzia Kituo cha Uridhi wa
Utamaduni Tanzania (TCCH) ambapo kupitia kituo hicho bidhaa mbalimbali za Sanaa
na Utamaduni zinauzwa ndani na nje ya nchi.
Akitoa pongezi hizo
kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo
hicho kutaiuza nchi, utamaduni wetu, kazi za sanaa na kuongeza ajira miongoni
mwa jamii yetu.
Aidha Profesa Gabriel
amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao na kushirikiana na wadau wote
ili kuhakikisha kwamba wanafikia mafanikio na malengo waliyojiwekea katika
uwekezaji huo.
Aliongeza kuwa ni
vyema sasa Kituo hiko kikafikiria kuanzisha vituo vidogo vidogo katika kanda
ili kurahishisha upatikanaji wa bidhaa hizo na kusaidi wasanii walioko
pembezoni wapate soko la bidhaa zao kwa Serikali ingependa kuona zaidi wasanii
wa ndani wakinufaika na uwepo wa Kituo hicho.
Pia ameuomba uongozi
wa Kituo hicho kuangalia namna ya kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwajengea uwezo wasanii hili kujenga soko
la uhakika,ubora na viwango vya hali ya juu.
Kwa upande wake Afisa
Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited Bw. Arif Sheikh ameishukuru Serikali kwa
kuonyesha ushirikiano kna imekuwa faraja kubwa kwao kwa kiongozi wa ngazi ya
juu Serikalini kukubali kuja kuzindua Kituo chao.
Sheikh amesema kuwa
kuanzishwa kwa Kituo hicho kumelenga kukuza sanaa na utamaduni wa Mtanzania
kwakuwa kinahusika na uuzaji wa bidhaa za sanaa na utamaduni tu, hivyo wasanii
wanayo fursa ya kujipatia kipato kwa kukiuzia Kituo kazi zao.
Hata hivyo Sheikh
alisema kuwa kutokana na ushauri uliotolewa Kampuni yao ipo tayari kutoa
ushirikiano zaidi kwa Serikali pindi watakapohitajika kufanya hivyo ikiwemoi
sualaua la kuwajengea uwezo wasanii wa kazi za mikono.
Kituo cha Urithi wa
Utamaduni Tanzaia ambacho kwa kingereza kinaitwa Tanzania Center for Cutural Heritage (TCCH) kipo katika jengo la Quality
Center, kinamilikiwa na Kampuni ya Qaulity Group Limited ya jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye suti nyeusi) akitembelea bidhaa mbalimbali za Sanaa na Utamaduni mara baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifurahia jambo na Mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume walipokutaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya picha kutoka kwa uongozi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kinamilikiwa na Kampuni ya Quality Group Limited.Kituo hicho ni duka ambalo linauza bidhaa za sanaa na utamaduni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya fimbo maarufu kwa jina la Rungu la Kimasai kutoka kwa Mshauri wa masuala ya bidhaa za sanaa na utamaduni Bibi. Caroline Kessy wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Utamaduni Tanzania (TCCH) kilichopo katika jengo la Quality Center leo jijini Dar es Salaam.
Post a Comment