MAAFISA USAFIRISHAJI WAASWA KUWA WAZALENDO.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akifungua kikao cha maafisa usafirishaji wa
Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi
Silivester Simfukwe na kulia ni Mhandisi Elirehema Mmari.
Na
Raymond Mushumbusi
mwambawahabariblog
Maafisa
usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali wameaswa
kuwa wazalendo kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matengenezo na shughuli za
kiufundi Serikalini.
Wito
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan alipokuwa akifungua kikao cha maafisa
usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali kujadili
changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni
zinazosimamia matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali.
Kaimu
Mtendaji Mkuu huyo amesema kwa hali ilivyo sasa imebainika kuwa Sheria na
Kanuni za matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali imekuwa ikikiukwa kwa
kiasi kikubwa na hivyo kuilazimu mamlaka husika kutafuta njia mbadala ili
kukabiliana na changamoto hiyo.
“Lengo
letu ni kupata namna bora ya kutoa huduma ya matengenezo ya kiufundi ya vifaa
vya Serikali pasipo kukiuka Sheria na Kanuni zilizowekwa hivyo basi tunaomba
ushirikiano kutoka kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuleta
magari na vifaa kwetu ili tutekeleze wajibu wetu” alisema Mhandisi Manase.
Mhandisi
Manase ameongeza kuwa pamoja na uchache wa Wizara , Idara na Taasisi za
Serikali zinazotekeleza Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari ya Serikali
kwa kuleta magari TEMESA ila kumekuwa na changamoto katika ulipaji wa gharama
za matengenezo hali inayosababisha Wakala usiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi Sylivester
Simfukwe amesema Wizara , Idara na Taasisi za Serikali zinatakiwa
kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo kwa kupeleka na kulipa gharama za
matengenezo ya magari na vifaa vya Serikali kwani Wakala huu ndio mshauri mkuu
wa Serikali katika masuala ya kiufundi na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo
itasaidia kuongezeka kwa mapato ya Serikali.
Naye
Meneja Usafirishaji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Jonathan
Mhagama ameiomba Serikali kuiongezea uwezo TEMESA kwa kuwa na karakana za
kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo kwa sasa
uwezo walionao wakala huo ni mdogo ukilinganisha na magari yaliyopo Serikalini.
Mkutano
kati ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na maafisa usafirishaji wa
Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za serikali umekuja mara baada ya kauli
kutoka kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame
Mbarawa ya kuyataka magari yote ya Serikali kutekeleza Sheria na Kanuni za
matengenzo ya vifaa vya Serikali.
Post a Comment