NAPE:NITARUDISHA HESHIMA YA TASNIA YA HABARI NCHINI.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa shinyanga Bi.Josephine Matiro akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye baada ya kuwasili mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za watumishi walio chini ya wizara yake na kuongea na wadau wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na watumishi wa serikali wa mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe(mwenye kofia ya njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage ambao unamilikiwa na chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi wa mkoa huo kutafta wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
.
Post a Comment